December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kikokotoo chaondoka na Mkurugenzi SSRA

Spread the love

RAIS John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Dk. Irene Isaka. Anaripotu Yusuph Katimba…(endelea).

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa, Dk. Irene atapangiwa kazi nyingine.

Hatua hiyo imechukuliwa na Rais Magufuli muda mchache baada ya kufanya mkutano na wawakilishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, serikali na vyama vya wafanyakazi ambapo alionesha kutoridhishwa na mfumo mpya wa kikokotoo.

Mfumo wa awali ukiruhusu mstaafu kuchukua asilimia 50 kwa mkupuo kisha zilizobaki akiendela kupewa kidogo kidogo.

Mfumo wa Sasa ulijielekeza kutoa kwa mkupuo asilimia 25 jambo ambalo lilikuwa likilalamikiwa.

error: Content is protected !!