Tuesday , 3 October 2023
Home Habari Mchanganyiko Prof. Muhongo awakalia kooni REA
Habari Mchanganyiko

Prof. Muhongo awakalia kooni REA

Fundi umeme wa Tanesco akiunganisha umeme wa REA katika moja ya nyumba zilizopo kijijini
Spread the love

WAZIRI wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ameiagiza bodi mpya ya wakurugenzi wa Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini (REA) kuwakagua wakandarasi wote ambao wamepata tenda ya usambazaji wa umeme vijijini, anaandika Dany Tibason.

Mbali na kutoa agizo la kuwakagua wakandarasi pia REA wametakiwa kuhakikisha wanatumia vifaa vinavyozalishwa ndani ambavyo vina ubora badala ya kuagiza vifaa vya umeme kutoka nje ya nchi.

Akizungumza na wajumbe wapya wa Bodi mpya REA, Prof. Muhongo amesema bodi hiyo inatakiwa kuwa na malengo mapana kwa ajili ya kuhakikisha umeme unawafikia wananchi kwa kiwango kikubwa.

Prof. Muhongo amewataka wajumbe hao wa bodi kuhakikisha wanapokea makablasha kabla ya wiki mbili ili waweze kuyapitia mapema na kuyasoma.

Katika kuhakikisha umeme unakuwa kichocheo cha maendeleo ni vyema umeme huo ukawekewa katika taasisi mbalimbali ili kuwapatia umeme.

“Sasa katika kutekeleza umeme unakuwa kichocheo, ni vyema umeme usivuke taasisi mbalimbali kama vile, shule zote za sekondari na shule za msingi, zahanati hospitali, mashamba makubwa na katika sehemu za kibiashara,” amesema.

Katika uzinduzi huo Prof. Muhongo, ameitaka bodi hiyo kuhakikisha inasimamia zaidi ubora wa vifaa vya umeme ambavyo vina ubora.

“Nawaagiza nyie bodi kuhakikisha mnaponunua vifaa vya umeme kuhakikisha vinakuwa na ubora na vinavyozalishwa,” amesema Prof. Muhongo.

Aidha amesema makampuni yote ya kutoka nje ya nchi ambayo yanafanya kazi ndani ni lazima kuwa na wakandarasi wadogo wa ndani na si vinginevyo.

“Haiwezekani kwa mfano nguzo za umeme zinapatikana hapa Iringa, lakini unaweza kushanga eti nguzo zinaagizwa kutoka Afrika Kusini na maeneo mengine,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wawili wanaswa wakitengeneza noti bandia

Spread the loveJESHI la Polisi mkoani Songwe limewakamata watu wawili kwa tuhuza...

AfyaHabari Mchanganyiko

Chanjo mpya ya malaria Sh 5,000-10,000

Spread the loveShirika la afya la Duniani (WHO) limeridhia chanjo ya pili...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wagonjwa kiharusi waongezeka, Hospitali Mkapa yaja matibabu mapya

Spread the loveHOSPITALI ya Benjamini Mkapa kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka...

Habari Mchanganyiko

Wananchi waamua kujenga zahanati kukwepa adha kufuata huduma mbali

Spread the loveWANANCHI wa Kijiji cha Kwikerege, kilichopo katika Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!