June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Prof. Mbarawa awatoa hofu wananchi Shinyanga

Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Spread the love

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewatoa hofu wananchi wa Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga kwamba hakuna mtu atakayechukuliwa ardhi yake bila kulipwa, anaandika Mwandishi Wetu

Amesema serikali haitamuonea mwananchi yeyote kwa wale ambao maeneo yao yatapitiwa na miradi mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya kiuchumi.

Waziri amesema kila mmoja atalipwa fidia kwa mujibu wa sheria ili kuipisha miradi hiyo ambayo itaisadia Tanzania kufikia kwenye uchumi wa kati mwaka (2025).

Mbarawa aliyazungumza hayo mjini Shinyanga kwenye ziara yake fupi ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inasimamiwa na wizara anayoingoza.

Amesemma serikali imedhamiria kujenga na kufufua miundombinu yake yote ya kiuchumi, ukiwamo huo uwanja wa ndege na bandari ya Isaka wilayani Kahama, miradi ambayo itasaidia kukuza sekta ya uchumi.

error: Content is protected !!