Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bendera azifunda halmashauri zake Manyara
Habari Mchanganyiko

Bendera azifunda halmashauri zake Manyara

Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Manyara
Spread the love

HALMASHAURI ya Wilaya ya Simanjiro, imeendelea kupata hati safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG), kwa mwaka wa saba mfululizo, anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumza wakati wa uwasilishwaji wa taarifa ya CAG ya mwaka wa fedha wa 2015/2016, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, aliitaka halmashauri hiyo kutobweteka baada ya kupata hati safi badala yake waongeze juhudi zaidi.

Amesema pamoja na kuipongeza halmashauri ya wilaya kwa kupata hati safi hataki kuona kwenye mkoa wake halmashauri isiyotunza hesabu zake ipasavyo na kusababisha kupata hati chafu au yenye mashaka.

“Kwenye mkoa wangu sitaki kuona halmashauri yenye kufanya mambo ya hovyo hovyo, hivyo endapo kuna viongozi ambao wanadhani watafanya kazi kwa mazoea watafute mkoa mwingine wa kwenda na siyo Manyara,” amesema

Amesema viongozi wa halmashauri hiyo wanapaswa kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakamilishwa kwa wakati na kutekelezwa kwa ubora na kutunza vyema taarifa za fedha ili kuendelea kupata hati safi.

“Mnapaswa kutambua siku za kufuja fedha zimepitwa na wakati na kwa wale viongozi ambao bado wanafanya kazi kwa mazoea badala ya kutumia jamii inawalazimu wajichimbie shimo na kujifukia,” amesema

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Jackson Sipitieck, amesema kwa muda wa miaka saba mfululizo wameweza kupata hati safi na wanatarajia kuendelea kupata hati safi kwa miaka ijayo ya fedha kutokana na usimamizi mzuri wa fedha waliojiwekea katika kusimamia miradi ya maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!