Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Mbarawa atembelea banda la TMA, aelezwa umuhimu wa taarifa za hali ya hewa
Habari Mchanganyiko

Prof. Mbarawa atembelea banda la TMA, aelezwa umuhimu wa taarifa za hali ya hewa

Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa jana alitembelea banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na kupata maelezo mbalimbali ikiwa pamoja na kuelezwa umuhimu wa taarifa za hali ya hewa katika misimu tofauti tofauti. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Waziri Mbarawa alitembelea banda hilo katika maonesho yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa lengo la kutangaza kazi za taasisi mbalimbali zilizopo chini ya wizara hiyo kupitia mkutano wa 15 wa wadau wa kutathmini utendaji kazi wa sekta ya uchukuzi kwa mwaka mmoja, uliofanyika katika ukumbi wa Kisenga LAPF – Dar es Salaam.

Prof. Mbarawa aliambatana na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Africa (AFDO) Dk. Patricia Laverley, pamoja na mambo mengine walielezwa umuhimu wa huduma za hali ya hewa kwa sekta ya ujenzi na uchukuzi ikiwa ni pamoja na huduma mahususi za usafiri wa barabara, maji na anga.

Aidha, kupitia maonesho hayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Wilbert Muruke alielezea umuhimu wa huduma za hali ya hewa katika sekta ya uchukuzi jinsi zinavyosaidia katika kutekeleza majukumu ya sekta vilevile kukabiliana na athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa.

“Kama mnavyoelewa huduma za hali ya hewa ni mtambuka kwa sekta mbalimbali mojawapo ya sekta ambayo tunaihudumia ni sekta ya usafirishaji ambapo katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo viwanja vya ndege, reli, barabara na madaraja moja ya taarifa muhimu katika mipango yao ni taarifa za hali ya hewa zitakazowawezesha kupanga vyema mipango yao na hivyo kusaidia kuepusha hasara zitakazojitokeza kutokana na majanga yatokanayo na hali mbaya ya hewa,” alisema Muruke.

Muruke aliongezea kwa kuwataka wadau kuendelea kufuatilia taarifa mbalimbali za hali ya hewa zinazotolewa mara kwa mara na TMA hususani katika kipindi hiki ambacho dunia imeendelea kukumbwa na mabadiliko ya hali ya hewa, kwani itasaidia kupunguza au kuepusha hasara zinazoweza kujitokeza kutokana na hali mbaya ya hewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!