Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Barabara ya kulipia Kibaha-Chalinze-Morogoro yaja
Habari Mchanganyiko

Barabara ya kulipia Kibaha-Chalinze-Morogoro yaja

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa
Spread the love

 

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema Serikali imejipanga kushirikiana na sekta binafsi katika ujenzi wa barabara mpya ya Kibaha-Chalinze-Morogoro yenye urefu wa kilomita 215 (express way) ambapo mkandarasi atajenga kwa fedha yake na watakaotumia barabara hiyo watalipia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Pwani … (endelea).

Amesema hatua hiyo inatokana na umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa miundombinu ili kuharakisha maendeleo na kukuza uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja.

Akifungua mkutano wa 15 wa mwaka wa wadau wa sekta ya uchukuzi wenye lengo la kufanya tathmini kuhusu maendeleo ya sekta hiyo nchini, Prof. Mbarawa amesema ushiriki wa sekta binafsi, Serikali na wadau wa maendeleo utaharakisha ujenzi wa reli, barabara, viwanja vya ndege na meli na hivyo kutoa fursa nyingi za ajira na kuhuisha miundombinu ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa.

Amebainisha kuwa Serikali inajipanga kubadilisha sheria ya TAZARA na TRC ili kuwezesha sekta binafsi kushiriki katika huduma ya usafiri wa reli kwa kununua mabehewa na kuyaendesha.

Amezungumzia umuhimu wa Tanzania kuwa na miundombinu bora kwa haraka ili kumudu kuhudumia kikamilifu soko la ndani na nchi sita ambazo hutegemea huduma ya uchukuzi kutoka Tanzania, ambazo ni Malawi, Zambia, Burundi, Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Kingdom Mbangula akizungumzia ujenzi wa barabara mpya ya kulipia, amesema barabara hiyo itakuwa na njia nne, mbili kwenda Morogoro na Mbili kurudi Kibaha na magari hayatapishana ili kuepusha msongamano na ajali.

“TANROADS tumejipanga ipasavyo kuhakikisha mradi huu unajengwa kwa ubora uliokusudiwa na kukamilika kwa wakati,” amefafanua Eng. Mbangula.

Naye Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley ameishukuru Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi  kwa kuandaa mkutano huo wa tathmini wa kila mwaka ambao unaibua changamoto na kuzipatia ufumbuzi kwa haraka.

Amesisitiza kuwa AfDB imetenga asilimia 60 ya bajeti yake katika uwezeshaji ujenzi wa miundombinu ili kuchochea maendeleo ya uchumi kwa nchi za Afrika.

Katibu Mkuu sekta ya Uchukuzi Bw. Gabriel Migire amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utaibua hoja mbalimbali zinazolenga kuboresha sekta ya uchukuzi nchini hivyo kuvutia wawekezaji wengi kupitisha mizigo yao Tanzania na hivyo kukuza uchumi wa taifa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

error: Content is protected !!