Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof.Lipumba: Njia ya Ikulu nyeupe
Habari za Siasa

Prof.Lipumba: Njia ya Ikulu nyeupe

Spread the love

PROFESA Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), amesema njia ya kuingia Ikulu ipo wazi. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni, Ilala jijini Dar es Salaam leo tarehe 13 Agosti 2020 Prof. Lipumba amesema, umati wa watu waliompokea umeonesha mapenzi kwake na hivyo kufungua njia ya kuingia Ikulu baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.   

Prof. Lipumba amerejea leo jijini Dar es Salaam akitoka kutoka kuchukua fomu za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC), Dodoma tarehe 11 Agosti 2020.

Akizungumza na mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye ofisi za CUF Prof. Lipumba amesema, umati wa watu waliojitokeza kumpokea umemrahisishia njia ya kuingia Ikulu.

“Nashukuru sana kwa mapokezi haya. Mapokezi haya yananipa moyo na njia ya kwenda Ikulu ya Dar es Salaam na ya Dodoma ambayo sasa iko wazi. Jukumu letu tujipange kwenye uchaguzi,” amesema Prof. Lipumba.

Amesema, kusudio la CUF tangu mwanzo la kutaka kubadilisha maisha ya Watanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, miundombinu na ajira bado lipo palepale.

Amesema, kwa sasa ndani ya nchi hakuna mzunguko wa fedha na kusababisha maisha kuwa magumu “hakuna mzunguko wa fedha ndani ya nchi. Tunahitaji kuongeza mzunguko wa fedha, kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji, biashara na ujasiriamali.

“Tunahitaji kuwekeza katika afya ya kina mama, afya ya watoto, elimu iliyo bora. Lakini ili tuyafanye haya yote, sisi kama Chama cha CUF ikiwa Watanzania watatupa ridhaa, tutaanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.”

Amesema, Serikali ya Umoja wa Kitaifa itasaidia kuhakikisha misingi ya demokrasia ambayo watu wanapigania kwa muda mrefu, inafikiwa.

Mamia ya wanachama na washabiki wa chama hicho, walianza msafara wa kumpokea Prof. Lipumba Ubungo Kibo kupitia Barabara ya Morogoro, Lumumba, Uhuru hadi kwenye ofisi za chama hicho Buguruni.

Msafara huo ulianza saa 6:20 mchana na kuhitimishwa saa 9:24 alasiri kwenye ofisi za chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!