Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yateua wagombea ubunge, uwakilishi Z’bar
Habari za Siasa

Chadema yateua wagombea ubunge, uwakilishi Z’bar

Bendera ya Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) visiwani Zanzibar, kimeteua wagombea 30 kati ya 50 wa ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktona 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea)

Kati ya majimbo 264 ya ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zanzibar ina majimbo 50 na Tanzania bara 214.

Taarifa ya Kado salmin Mwalimu, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni na Uchaguzi wa Chadema Ofisi ya Makamu Makuu Zanzibar imesema, chama hicho pia, kimeteua wagombea uwakilishi 21.

Kati ya wagombea hao 30, wanaume ni 22 na wanawake n inane huku kati ya 21 wa uwakilishi, wanawake ni wawili na wanaume ni 19.

Kwa upande wa Tanzania Bara, Chadema imekwisha kuteua majina 200 ya wagombea na kubaki 14.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-bara, Benson Kigaila amezungumza na MwanaHALISI Online leo Alhamisi tarehe 13 Agosti 2020 kuhusu majimbo hayo 14 yaliyobaki ambapo amesema yatatangazwa katika awamu ya tatu.

Kigaila amesema, awamu ya kwanza walitoa orodha ya wagombea 163, awamu ya pili 37 na majimbo hayo 14 baadhi wanarudia kura za maoni kutokana na rufaa zilizokuwa zimewasilishwa.

Amesema, majina ya wagombea kwenye majimbo hayo yatakuwa tayari kabla ya tarehe 19 Agosti 2020.

Tayari shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za ubunge na udiwani zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 5-25 Agosti 2020.

Kampeni za uchaguzi huo zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!