Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Hoseah aanika mafanikio aliyofanya TLS, aomba achaguliwe tena
Habari Mchanganyiko

Prof. Hoseah aanika mafanikio aliyofanya TLS, aomba achaguliwe tena

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), anayetetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah
Spread the love

 

RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), anayetetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah, amesema katika kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kuimarisha mahusiano kati ya chama hicho na Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mgombea huyo urais wa TLS kwa awamu ya pili, ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 27 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam, katika mdahalo wa wagombea urais wa chama hicho. Wengine ni, Jeremiah Mtobesya na Harold Sungusia.

Prof. Hoseah amesema, kufuatia kuimarika kwa mahusiano hayo, Serikali imekubali kutenga Sh. 1.4 bilioni, kwa ajili ya ruzuku kwa TLS katika utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi.

“Nimeshaongea na Serikali nasubiri bajeti ambayo inaanza mwezi wa June, Wizara ya Katiba na Sheria imekubali kutenga Sh. 1.4 bilioni kwa ajili ya ruzuku katika zoezi la kusaidia misaada ya wananchi. Sababu TLS inatekeleza jukumu la umma,” amesema Dk. Hoseah.

Prof. Hoseah amesema, amefanikiwa kuishawishi Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kusaidia uendeshaji wa Kituo cha Usuluhishi cha Kimataifa Tanzania, ambapo imekubali kutoa kiasi cha Sh. 1.2 bilioni.

“Serikali ilitaka migogoro ya kibiashara itatuliwe nchini, imekubali kutoa fedha kusaidia kituo Sh. 1.2 bilioni, ili tuweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na jambo hili sio geni, wale wanaofikiria kuhongwa na Serikali si sahihi,” amesema Prof. Hoseah.

Pia, Prof. Hoseah amesema katika kipindi cha uongozi wake amefanikiwa kuishawishi Mahakama Kuu ya Tanzania, kurejesha tozo za ada zinazotolewa na mawakili kiasicha Sh. 450, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa wakati akigombea nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa mwaka jana.

“Tumerudishiwa Sh. 450 milioni, ambazo tangu uhuru tulikuwa tukilipa mahakama kama ada, hatujawahi kurudishiwa. Kwa uongozi wangu zimetengwa Sh. 450 milioni, sasa jamani mnataka tufanyeje? Mimi sio wa blab la ni wa vitendo, nimetekeleza,” amesema Dk. Hoseah.

Akitaja mafanikio mengine, Prof. Hoseah amesema amefanikiwa kutekeleza ahadi yake ya kupunguza gharama ya bima ya afya, kutoka Sh. 1,050,000 hadi kufikia 500,000.

“Niliahidi mawakili wenye ulemavu kwamba tutashirikiana, niliahidi kuongea na mahakama katika mpango mkakati wa kuweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu na hili limetekelezwa na mahakama,” amesema Prof. Hoseah.

Prof. Hoseah amesema, amefanikiwa kupunguza tozo ya ada ya uwakili kutoka Sh. 60,000 hadi 20,000, huku akijinasibu kwamba, wakati wa uongozi wake hakuna wakili aliyefukuzwa au kusimamishwa kwa sababu mbalimbali.

Mgombea huyo Urais wa TLS, amewaomba mawakili wamchague ili aendelee na majukumu aliyoyaacha pamoja na mengine mapya aliyopanga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!