Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wawatahadharisha wakazi wa Monduli
Habari za Siasa

Polisi wawatahadharisha wakazi wa Monduli

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, SACP Ramadhani Ng’anzi
Spread the love

IKIWA kesho tarehe 16 Septemba 2018 ni siku ya uchaguzi mdogo katika majimbo mawili na kata zaidi ya 20 za Tanzania Bara, Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewatahadharisha wananchi wa jimbo la Monduli kutofanya fujo ili kukwepa kuchukuliwa hatua. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, SACP Ramadhani Ng’anzi wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 15 Septemba 2018, ametoa onyo kwa wanaopanga kufanya fujo kesho katika uchaguzi, akisema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo liko imara.

“Ole wao watakaopanga kufanya vurugu, Jeshi la Polisi lipo imara na halitashindwa kumkamata yeyote atakayeshawishi au kufanya fujo katika uchaguzi huo ambao tunategemea utakuwa wa amani na utulivu,” Amesema Kamanda Ng’anzi.

Aidha, amewataka wananchi wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo, na kisha kurudi kwenye makazi yao baada ya kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura ili kuepusha vitendo vya vurugu.

Kamanda Ng’azi amewahakikishia wananchi kuwa, Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi ili uchaguzi huo ufanyike kwa amani na utulivu.

“Kama ilivyo kwenye kampeni hali ilikuwa tulivu na wakati wa uchaguzi tutahakikisha kwamba hali hii inaendelea kuwa shwari, askari toka vikosi mbalimbali watakuwepo wilayani hapo kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika hali ya usalama.” Amesisitiza Kamanda Ng’anzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!