Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Polisi wavamia mkutano wa Zitto
Habari za Siasa

Polisi wavamia mkutano wa Zitto

Spread the love

MAOFISA kutoka Jeshi la Polisi limevamia Makao Makuu ya Chama cha ACT-Wazalendo na kuondoka na Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi na Uenezi. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo tarehe 16 Agosti 2019, siku ambayo Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama hicho alipanga kufanya mkutano na wanahabari kwa ajili ya kuzungumzia Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Kabla ya mkutano huo kuanza, polisi waliovaa mavazi ya kiraia wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni RCO, John Malulu waliwatawanya waandishi wa habari waliokuwa wanasubiri mkutano huo uliotarajia kuanza saa tano asubuhi.

RCO Malulu aliwatawanya wanahabari pasipo kuwaeleza sababu za kuchukua uamuzi huo.

“Naomba waandishi mtawanyike hili jambo linalotakiwa kufanyika lisimame, nadhani nimeeleweka,” RCO Malulu aliwaambia waandishi.

Kabla ya kukamatwa, Ado aliwaeleza wanahabari kwamba polisi waliwataarifu kwamba, wanahitaji kiongozi yeyote wa chama chao kufika katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay kwa ajili ya mahojiano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!