DAKTARI Mohmmed Seif Katibu, aliyewahi kuwa Mkuu wa Oganizesheni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nyakati tofauti, amefariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Tayari taarifa za kifo hicho zilizotolewa na familia yake leo Jumatatu tarehe 15 Februari 2021, zimeeleza Mzee Seif alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Al Rahma, Kilimani visiwani Zanzibar mpaka mauti yanamkuta, mapema leo asubuhi.
Mzee Seif Khatibu mapaka anafikwa na mauti, alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) na mmiliki na Mkurugenzi wa Zanzibar Media Group inayomiliki Kituo cha Redio cha Zenj FM, TV na Gazeti la Nipe Habari,
Katika maisha yake ya siasa, Mzee Seif Khatibu alikuwa Mtu wa karibu na mtiifu kwa Mwalimu Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania, alikuwa mjumbe katika Juuiya ya Umoja wa Vijana Tanzania (UVT) kabla ya kubadilisha na kuwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM).
Mzee Khatibu aliwaki kuongoza wizara mbalimbali Bara na Visiwani ambapo pia aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Uzini, Zanzibar
Pia, aliuwa mshairi na Mhadhir katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Aliwahi kuwa mwanasoka aliyechezea Klabu ya Kikwajuni Sport na Timu ya Taifa ya Zanzibar. Mzee Seif Khatibu pia aliwahi kuimba taarabu.
Mwaka 2015, wakati wa mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za wagombea urais ndani ya CCM, Dk. Khatibu akiwa, Mkuu wa Oganizesheni wa chama hicho, alikuwa na jukumu la kuwapatia fomu wagombea wote waliojitokeza zaidi ya 38 akiwemo, Dk. John Pombe Magufuli, ambaye baadaye aliibuka mshindi wa Urais.
Dk. Khatibu amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashuari Kuu ya CCm, kati ya mwaka 1978 hadi 2017, Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hichokati ya mwaka 1995 hadi 2017) na baadaye akwa katibu wa Oganaizesheni kati ya 2012 na 2017.
Khatibu, alikuwa mtunukiwa wa kwanza wa shahada ya uvamivu (PhD), katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), tarehe 25 Novemba 2011 na alitunukiwa shahada hiyo na aliyekuwa mkuu wa chuo hicho, Hayati Benjamin Willim Mkapa.
Changamoto ya kupumua? Au Covid 19? Siku zote mnatuambia eti msema kweli ni mpenzi wa …….