PROFESA Mark Mwandosya, waziri wa zamani katika utawala wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, ameeleza kuumizwa na kifo cha baba yake mdogo, Agen Mwandosya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Taarifa ya msiba huo imetolewa na Prof. Mwandosya leo Jumatatu tarehe 15 Februari 2021, kupitia ukurasa wake wa twitter.
Kwenye taarifa hiyo, Prof. Mwandosya ameeleza baba yake amefariki alfajiri ya kuamkia leo kutokana na changamoto ya upumuaji akieleza kuwa ni corona.
“Nasikitika kuwatangazia kifo cha baba yangu mdogo, Agen Mwandosya, kilichotokea alfajiri ya leo baada kupata ‘changamoto ya kupumua’, kwa jina jingine Corona au Covid 19,” ameandika.
Kwenye tangazo hilo, Prof. Mwandosya amesema, itakuwa pole na faraja kwao kama tangazo hilo litasaidia kuokoa maisha ya watu wengine.
“Kama tangazo hili litasaidia kuokoa maisha ya Mtanzania hata mmoja tu, itakuwa pole tosha na faraja kwetu,” ameandika.
Asante Profesa kwa kuwa mkweli na wazi. Umetaja ugonjwa ni Covid 19 badala ya kumung’unya maneno kama wafanyavyo Bakwata na madaktari ambao wanakataa kutaja jina la ugonjwa na kusema UPO