Saturday , 4 February 2023
Home Kitengo Michezo Nusu Fainali FA Cup, Yanga, Biashara United watambiana
Michezo

Nusu Fainali FA Cup, Yanga, Biashara United watambiana

Spread the love

 

Kuelekea mchezo wa kesho wa nusu fainali ya michuano ya kombe la FA (Azam Federation Cup) kati ya Yanga dhidi ya Biashara kutoka Mara, makocha wa pande zote mbili wametamba kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo, kila mmoja akijiamini kwa kikosi chake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza utapigwa kesho kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora majira ya saa 9:30 jioni.

Kwa upande wa Yanga, kocha wa makipa wa kikosi hiko Razak Siwa amesema kuwa wachezaji wote wapo vizuri kwa mchezo huo, na wana hali ya kuibuka na matokeo.

“Tumejiandaa vizuri sana kwa mechi ya kesho, wachezaji wote wapo wanahali nzuri, na majeruhi wapo ila tumewacha Dar es Salaam, wengine wapo vizuri.” Alisema Siwa

Aidha kocha huyo pia alitoa ufafanuzi wa kwanini katika michezo ya hivi karibuni, kikosi hiko kina ruhusu sana mabao hasa kwenye michezo ya Ligi, licha ya kuondoka na ushindi.

“Tatizo la kuruhusu magoli tunalifanyia kazi, lakini ni gumu sana, lakini kwa sasa tunapigania kupata ushindi kuanzia mchechi ya kesho na zilizosalia ili kujiweka sehemu nzuri.” Aliongezea kocha huyo

Kwa upande wa kocha wa Biashara United Patrick Okumu raia wa Kenya alisema kuwa, wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo huo dhidi ya Yanga, licha ya kukili kuwa utakuwa mchezo mgumu.

Tumejaindaa vizuri na wachezaji wote wapo, hatuna majeruhi na hali ipo juu, na wapo tayari kucheza mchezo huo dhidi ya Yanga, najua utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa mechi hiyo.” Alisema kocha huyo

Biashara United walifanikiwa kufuzu kwenye hatua hiyo ya Nusu fainali, mara baada ya kuiondosha Namungo FC, kwa jumla ya mabao 2-0, kwenye mchezo wa Robo fainali.

Kwa upande wa Yanga wametinga hatua hiyo ya nusu fainali, mara baada ya kuiondosha Mwadui Fc, kwenye mchezo wa robo fainali kwa mabao 2-0, kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Ccm Kambarage Shinyanga.

Katika michezo miwili waliokutana kwenye Ligi Kuu kwa msimu huu, Yanga amefanikiwa kuondoka na ushindi katika michezo yote.

Hii ni mara ya pili kwa Yanga kufuzu hatua hiyo ya nusu fainali, katika kipindi cha misimu miwili mfululizo, katika msimu wa 2019/20 Yanga iliondoshwa kwenye hatua hiyo mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1, dhidi ya Simba.

Katika dakika 90 za mchezo huu wa leo, kama timu hizo zikitoka sare, zitakwenda kwenye muda wa nyongeza (Dakika 120) na kisha mikwaju ya Penati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!