July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakazi ataka mchakato Katiba Mpya uendelee

Spread the love

 

MSANII wa HipHop nchini Tanzania, Webiro Wakazi Wassira maarufu ‘Wakazi,’ amesema ni muhimu kuhuisha mchakato wa Katiba Mpya. Anaripoti Matilda Peter…(endelea).

Amesema, anatamani kuona mchakato wa Katiba Mpya unarejea ili maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume ya Jaji Joseph Warioba (Mwenyekiti wa Tume), yanafanyiwa kazi.

“Ni muhimu kwa nchi inayohitaji maendeleo kuangalia mchakato wa Katiba Mpya. Nchi inaongozwa na Katiba iliyo huru, Katiba ya Wananchi itasaidia sana kusukuma maendeleo,” amesema Wakazi wakati wa mahojiano na MwanaHALISI TV na Online.

Msanii huyo amesema, Tanzania ina kila sababu ya kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya, hasa kwa kutumia maoni ya wananchi yaliyokusanywa awali.

Amesema, maoni ya wananchi katika Katiba Mpya, yalilenga kutoa mwongozo kwa viongozi na kufinya matumizi mabaya ya madaraka.

“Sasa ni wakati sahihi kuendelea na mchakato wa Katiba Mpya kwa maslahi ya Taznania na Watanzania,” amesema.

error: Content is protected !!