Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yawapa mchongo wafanyabiashara Temeke
Habari Mchanganyiko

NMB yawapa mchongo wafanyabiashara Temeke

Spread the love

 

WANACHAMA wa Klabu ya Wafanyabiashara wanaohudumiwa na Benki ya NMB, Wilaya ya Temeke (NMB Business Club) jijini Dar es Salaam, kutumia fursa zitokanazo na ongezeko la kiwango cha mikopo midogo ya kuanzia Sh. 500,000 hadi Sh.75 milioni na kushuka kwa riba zake kutoka asilimia 21 hadi asilimia 14, ili kujiimarisha kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, wakati wa kongamano lililoshirikisha wanachama zaidi ya 150 wa NMB Business Club wilayani Temeke, lililofanyika ukumbi wa mikutano wa PR Hotel, jijini Dar es Salaam, ambalo lilifunguliwa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Ezekiel Gutti.

Akizungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali hao, Donatus alibainish, NMB ambayo ni benki kinara miongoni mwa mabenki zaidi ya 50 nchini, ina mtaji wa kutosha unaowapa wateja wao uhakika wa usalama wa fedha zao na usiri.

Alisema hiyo ndio imechangia zaidi ongezeko kubwa la kiwango cha mikopo midogo, sambamba na kushuka kwa riba za mikopo hiyo.

“Kiwango cha mikopo midogo midogo kinachoanzia Sh. 500,000 hadi Sh. Mil. 50, sasa kimepanda hadi kufikia Mil. 75, wito wetu kwenu ni endeleeni kutumia fursa hiyo muhimu ya mikopo, ambayo kwa wale wateja wanaochiupikia, riba imeshuka kutoka asilimia 21 ya awali na sasa kuwa asilimia 14. Huduma hizi zipo matawini, karibuni,” alisema.

“Mnachotakiwa kutambua tu ni ukweli kwamba ninyi mko katika benki sahihi, kwa sababu NMB tunaongoza wateja zaidi ya Mil. 4, hii ina maana mnahudumiwa na benki inayoaminiwa zaidi nchini. Tunaongoza pia kwa faida, na hii lazima tuwashukuru ninyi, kwani kupitia ninyi ndo tumeongoza faida hadi Desemba 2021 ya Sh. Mil. 289,” alisema.

Donatus aliwataka wanachama hao kuwa mabalozi wema wa NMB katika jamii inayowazunguka, ili kuongeza idadi ya wanufaika wa huduma mbalimbali, kama za bima, zikiwemo za vikundi vya kuanzia watu watano na kuendelea, ambazo zinatoa kinga na kutoa fidia kwa mwanachama na familia (mke/mume na watoto) anapofariki.

Kwa upande wake, Mtoa Mada Mkuu wa Kongamano, James Mwang’amba, aliwataka wafanyabiashara na wajasiriamali walioshiriki kongamano hilo kuhakikisha wanakata ‘minyororo isiyoonekana,’ ambayo imekuwa ikikwaza ustawi wa biashara na kuyumbisha ukuaji kibiashara na kiuchumi miongoni mwao.

Mwang’amba aliitaja ‘minyororo sita iyoonekana’ inayowakwamisha wengi wao kuwa ni pamoja na Kuamini kuwa mafanikio ni mchakato wa polepole, kuachana na dhana ya mtu kujiona ama kuamini hawezi, kuwaepuka ndugu, jamaa, marafiki na watu wa karibu wanaokatisha tama na kiwango kidogo cha uwezo wa kumiliki hisia hasi.

Minyororo mingine iliyotajwa na Mwang’amba katika Kongamano hilo lililowashirikisha pia wadau wa biashara wakiwamo Kikozi cha Zimamoto na Uokoaji, Kampuni za Bima ni tabia ya mtu kujaribu kumsaidia ama kumuokoa kila mtu anayezunguka na mwisho ni kukosa mfumo sahihi wa kiutendaji – ikiwemo uagizaji, uratibu, usimamizi.

Awali, akifungua kongamano hilo, Mwenyekiti wa NMB Business Club Wilaya ya Temeke, Ezekiel Gutti, aliwataka wanachama wake kuyatumia vema mafunzo yatakayo tolewa, ili kuharakisha ustawi wa biashara na kuimarika kiuchumi, pamoja na kuyaorodhesha mapendekezo yao kwa NMB ili yafanyiwe kazi na uongozi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!