Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia aeleza mafanikio kuanzishwa RUWASA
Habari za Siasa

Rais Samia aeleza mafanikio kuanzishwa RUWASA

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia amesema kumekuwepo na mafanikio makubwa katika sekta ya maji baada ya kuanzishwa kwa Mamlaka ya Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Samia ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 22 Machi 2022 wakati akifunga kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

“Mbali na serikali kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa miradi tulioa tufanye mabadiliko ya kimfumo ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi ya maji vijijini kwa kuanzisha wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa)”

Amesema kuanzishwa kwa Ruwasa kumerekebisha usimamzi wa miradi na kuongeza kasi ya utekelezaji wake na kwamba imeongeza nidhamu ya kazi na ufanisi wa kazi kwa wahandisi ambao sasa wapo chini ya Wizara ya maji baada ya kutolewa Tamisemi.

“Tofauti na ilivyokuwa hapo awali usimamizi wao ulikiwa mgumu lakini sasa mfumo huu umeleta matunda mazuri na kazi za maji zinakwenda vizuri hasa vijijini,” amesema.

Ameongeza kuwa hivi sasa wizara ya maji imeanza kuonesha mwelekeo mzuri na kazi wanazofanya zinaridhisha.

“Na ndiyo maana mageuzi ya Januari 2022 Wizara ya maji sikuigusa kabisa kwasababu ukiacha mageuzi niliyompa kibali Waziri nenda kaondoe, kabadilishe, kafukuze lakini huku juu sikugusa kabisa kwasababu niliona mwendo unakwenda vizuri,” amesema Rais Samia.

Hata hivyo Mkuu huyo wa nchi amesema natambua ipo miradi ya maji bado inasuasua kwamba ripoti ya EWURA itampa mwelekeo wa miradi inayosuasua na sababu zake ili kujua hatua za kuchukua.

Aidha amesema kuna tatizo katika kasi ya usambazaji wa kiradi ya maji kwa wananchi kwani miradi inakamilika kwenye maeneo lakini bado maji hayajapelekwa kwa wananchi.

“Kwahiyo watumishi wa mamlaka za maji msipumzike bado kuna kazi nendeni mkasambaze maji kwa wananchi,”amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!