Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Umoja wa Ulaya: Afrika iungane na dunia yote kuipinga Urusi
Habari Mchanganyiko

Umoja wa Ulaya: Afrika iungane na dunia yote kuipinga Urusi

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Nabil Hajlaoui
Spread the love

 

UMOJA wa Ulaya (EU) umetoa tamko la kuendelea kulaani kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine na kushawishi mataifa mbalimbali zikiwemo nchi za Afrika kuipinga Urusi kwa kitendo chake cha kuivamia Ukraine kijeshi. Anaripoti Erasto Masalu, Dar es Salaam … (endelea).

Tamko hilo limetolewa na baadhi ya mabalozi wa nchi za Ulaya waliopo nchini Tanzania ambao nchi zao ni wanachama wa EU, wakieleza kuwa kuungana huko hakutakuwa na maana Urusi itasitisha uvamizi muda huohuo lakini itakuwa na maana kubwa kwa kuionyesha Urusi jinsi dunia ambavyo haikubaliani nao.

Wakizungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam, leo Jumanne Machi 22, 2022 mabalozi hao wa Ufaransa, Ujerumani, Poland, Uholanzi, Sweden, Finland, Hispania, Italia na Balozi wa EU wamesema kuwa vikwazo vitaendelea kwa Urusi na washirika wake wote wanaojihusisha na vita hiyo kwa kuwa siyo jambo la kuachwa liendele.

Wamesema nchi za Afrika japo zipo ambazo hazijaweka wazi msimamo wao kuhusu kuchagua upande katika vita hiyo ikiwemo Tanzania ambayo haikutaja upande wake katika kura zilizopigwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA, lakini wanaamini kuwa hawafurahishwi na kinachoendelea nchini Ukraine kwa kuwa raia wengi wanaathirika.

“Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ambayo pia inajulikana kwa jina la Mahakama ya Dunia imeshatoa tamko la kuitaka Urusi kusitisha mapigano na kuondoa vikosi vyake Nchini Ukraine.

“Demokrasia, uhuru na haki za raia wa Uraine zinapotea, EU ina uwekezaji mkubwa katika Afrika kuliko Urusi. Tunajua Tanzania haikupiga kura ya kuchagua upande lakini haifurahishwi na kinachoendelea Ukraine,” anasema Balozi wa Ufaransa, Nabil Hajlaoui.

Balozi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Manfredo Fanti (katikati)

Balozi Hajlaoui anaongeza kuwa wa Ufaransa hawana nia ya kuchocheza vita wala uchagua upande lakini kuendelea kwa vita kutamaanisha kuwa watu wengi ambao hawana hatia watazidi kumia, pia nia yao ni vita imalizike kwa mazungumzo.

“Lakini kama vita itaendelea vikwazo vitaendelea kwa Urusi na washirika wake katika vita hiyo kwenye nafasi mbalimbali za kiuchumi na kwingineko,” anasema Balozi Hajlaoui.

Kwa upande wake Balozi wa Poland nchini Tanzania, Krzysztof Buzalski alisema: “Nchini kwetu tuna wakimbizi takribani milioni 2, takwimu zinaonyesha kuwa kama vita itaendelea inamaanisha kuwa wakimbizi wanaweza kufikia hadi milioni nane, hii ni kitu kibaya.

“Kuhusu madai ya uwepo wa ubaguzi kwa watu Weusi hatujapata taarifa hizo rasmi japo tulisikia, lakini kama kweli vitendo hivyo vipo basi tunalaani kwa nguvu zote.”

Naye Balozi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Manfredo Fanti amesema: “Tanzania inatambua maana ya kuwa na wakimbizi na imekuwa ikiwapokea kutoka nchi za jirani, kuna mamilioni ya watu wanateseka.

“Hii ndiyo maana EU imeamua kuweka bajeti ya kununua silaha kuisaidia Ukraine kujilinda. Tunategemea wafuasi mbalimbali wa UN wataunga mkono hiki kinachoendelea.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!