Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara NMB yageukia wakulima, Rais Samia awapongeza
Biashara

NMB yageukia wakulima, Rais Samia awapongeza

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi akitoa maelezo kwa Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea banda lao katika uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo leo Dodoma. NMB ni wadhamini na wadau wa kilimo. Rais amewapongeza kwa kazi nzuri
Spread the love

JUMLA ya Sh78. 8 bilioni zimeshatolewa na Benki ya NMB nchini Tanzania kwa wakulima kati ya Sh.100 bilioni walizotengewa kwa ajili ya kukopeshwa kwa riba nafuu ili kusaidia kukuza mnyororo wa kilimo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Fedha hizo ni sehemu ya mkakati wa NMB kwa ajili ya sekta ya kilimo inayoajiri Watanzania wengi zaidi ambapo benki inatoa fedha hizo kwa riba isiyozidi asilimia 10.

Takwimu hizo zilitolewa leo Jumatatu, tarehe 4 Aprili 2022 na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mpozi mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea banda la benki hiyo kinara nchini.

Ni wakati Rais Samia akizindua ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa ugani kilimo nchini humo katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Mponzi amesema kati ya Sh.100 bilioni zilizotengwa kukopeshwa kwa wakulipa kwa riba ya chini ya asilimia 10, zaidi ya Sh.78.8 bilioni zimeshakopeshwa kwa wanufaika 3,773 huku wakiwafikia zaidi ya wakulima na wajasiliamali wa kilimo milioni 1.4 kupitia taasisi yao ya NMB Foundation.

“Mbali na kiwango hicho, pia benki ya NMB imefanikiwa kuandaa mpango wa kufungulisha akaunti kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambapo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita zaidi ya akaunti 500,000 zilifunguliwa,” amesema Mponzi.

Afisa huyo amesema lengo la njia hiyo ni kuwawekea wakulima utaratibu maalumu ili wakidhi vigezo vya kupatiwa huduma za kifedha ikiwemo mikopo na mafunzo.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, mpango huo ni kuunga juhudi za serikali, katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo ya kiuchumi ya Vijana na Wanawake, hivyo waliamua kutangaza hati fungani maalumu tuliyoiita waliyoiita JASIRI BOND.

Hati hiyo imejikita katika kuwasaidia kusaidia wanawake wajasiliamali kwa riba nafuu ambapo mwitikio umekuwa mkubwa sana hata wameamua kuzindua NMB PESA lengo likiwa ni kurahisisha huduma za kipesa kwa wakulima na wateja wote kuwa karibu zaidi kwenye maeneo yao.

Akizungumzia utoaji wa mbegu za mafuta amesema, tayari wateja 332 wakiwemo wakulima katika vyama vya ushirika (AMCOS) wameshanufaika na zaidi Sh6 bilioni zimetolewa kwenye eneo hilo kama mikopo.

Nyingine ni kuwa benki hiyo imeshatoa zaidi ya Sh110 milioni kama mikopo ya bima ya afya za afya kwa makundi na taasisi za wakulima 697.

Baada ya juhudi za Serikali kutangazwa katika kuongeza uzalishaji wa mafuta nchini na kupunguza kiasi cha fedha kinachotumika kuagiza Mafuta nje, NMB wameshafanya mawasiliano na wizara ya kilimo ili kuunga mkono juhudi hizo na tayari wametengeneza muundo wa mikopo kwa wakulima na mnyororo thamani unaeleza jinsi ya kuwasaidia wakulima.

Kwenye sekta ya mikopo, NMB kwa kipindi cha miaka mitano wameshakopesha zaidi ya Sh1.3 trilioni kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji na minyoyoyo yote ya thamani.

Kingine ni kuwa, wameshaandaa mpango wa kufungulisha akaunti kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambapo kwa miaka miwili iliyopita, zaidi ya akaunti 500,000 zilifunguliwa.

Mara baada ya kupokea maelezo hayo, Rais Samia amewapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

Biashara

420 Blaze It chimbo jipya la kuchota mihela Meridianbet kasino 

Spread the love  JE, umewahi kucheza mchezo wa droo wenye droo 10?...

Biashara

Exim yawainua kiuchumi wanawake wajasiriamali kupitia mpango wa WEP

Spread the love  BENKI ya Exim kupitia Mpango wake wa Kuwawezesha Kiuchumi...

error: Content is protected !!