Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB kuanza kusajili wanachama Yanga Julai 10
BiasharaMichezo

NMB kuanza kusajili wanachama Yanga Julai 10

Spread the love

BENKI ya NMB kupitia matawi yake yote nchini inatarajiwa kuanza rasmi Jumatatu tarahe 10 Julai 2023, kusajili na kutoa kadi za uanachama wa Klabu ya Yanga. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 8 Julai 2023 na Idara ya Mawasiliano ya benki hiyo, mwanachama wa Yanga akifungua akaunti atalipia Sh. 34,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga (Sh. 5,000 ni malipo ya kadi, Sh. 5,000 amana ya kuanzia na Sh. 24,000 ni ada ya mwanachama kwa mwaka mzima).

Taarifa hiyo imeeleza kuwa mwanachama wa Yanga  atalipia Sh. 29,000 kama kianzio cha kupata kadi ya Yanga ambayo ni kadi ya malipo ya kabla (Prepaid Card) Sh. 5,000 ni malipo ya kadi na Sh. 24,000 ni ada ya mwanachama kwa mwaka mzima).

“Kadi hizi hazitakua za uanachama/ushabiki tu, pia zina uwezo wa kufanya kazi kama kadi ya Benki! Unaweza kufanya miamala yote ya kibenki ikiwemo kuiwekea pesa, kutoa hela katika ATM na kufanya malipo mtandaoni na katika vituo vya malipo (POS).

“Wanachama wanaweza kupata kadi za malipo ya kabla ambayo huitaji kuwa na akaunti nasi na kufanya malipo kwa kupitia mtandao au kwenye Point of Sales (POS),” imeeleza taarifa.

Aidha, imefafanuwa kuwa wanachama wa Yanga watanufaika na huduma na ofa mbalimbali za NMB ikiwemo mikopo isiyokua na dhamana (Mshiko Fasta) na punguzo la bei wakifanya malipo kupitia NMB Lipa Mkononi (QR).

Mbali na huduma za uanachama, NMB itaanzisha bima ya mwananchi ambayo itakua na gharama nafuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

error: Content is protected !!