Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Balozi Karume: Sikati rufaa kufukuzwa CCM, uamuzi ni batili
Habari za SiasaTangulizi

Balozi Karume: Sikati rufaa kufukuzwa CCM, uamuzi ni batili

Spread the love

BALOZI Ali Karume amedai uamuzi kumvua uanachama uliochukuliwa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni batili hivyo hana haja ya kukata rufaa kuupinga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).

Balozi Karume ametoa kauli hiyo akizungumza na MwanaHALISI Online, leo tarehe 8 Julai 2023,  ikiwa ni saa kadhaa  tangu Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja, kutangaza kumvua uanachama na kumtaka arejeshe kadi.

Mwanasiasa hiyo amedai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM kwa kuwa kikao kilichotoa uamuzi huo kilikuwa batili kwa kukosa mwenyekiti halali.

“Sina haja ya kukata rufaa kwenye uamuzi batili. Maamuzi hayakufanyika kwenye kikao halali kwa kikao kukosa Mwenyekiti halali,” amesema Balozi Karume.

Kikao hicho kiliketi chini ya Katibu wa CCM Kusini Unguja, Amina Mnacho na uamuzi wake kutangaza na Katibu Mwenezi wa Chama hicho Mkoa wa Kusini Unguja, Ali Timamu Haji.

Balozi Ali alihojiwa na Kamati za Maadili ya CCM kuanzia ngazi ya Tawi la Mwera, Jimbo la Mwera na Wilaya ya Kati, Kisha alipewa barua ya onyo huku akiwekwa chini ya uangalizi wa miezi mitatu.

Balozi Karume amepewa adhabu hiyo kwa madai ya mienendo yake kukiuka maadili ya CCM, ikwiemo kukituhumu kwamba hakina demokrasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!