Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nimewakimbia Chadema, hawashauriki – Mgeja
Habari za Siasa

Nimewakimbia Chadema, hawashauriki – Mgeja

Spread the love

ALIYEKUWA kada wa miaka mingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamis Mgeja, ambaye miaka miwili iliyopita, alikihama chama hicho na kutimkia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumfuta Edward Lowassa, amerejea tena kwenye chama hicho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Amedai kuwa sababu yeye kurejea CCM, kunatokana na Chadema kutoshaurika na utekelezaji mzuri wa ahadi alizotoa Rais John Pombe Magufuli, kwenye uchaguzi mkuu uliyopita. 

Mgeja ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Machi 2019, jijini Dar es Salaam katika mkutano wake na waandishi wa habari, uliofanyika kwenye hoteli ya Lamada.

Amesema, wakati alipojiunga na Chadema alikuta baadhi ya mambo hayako sawa na hivyo akashauri kurekebishwa, lakini hakuna aliyemsikiliza.

Miongoni mwa aliyodai kuwa hayako sawa, ni pamoja na chama hicho kuwa chama cha kiharakati, badala ya kuwa chama cha siasa.

 Alisema, “tulipoamua kujiunga na Chadema, tulikuta baadhi ya mambo hayako sawa. Tukashauri tutoke kwenye chama cha harakati na kuwa chama cha siasa; lakini wakatupuuza. Tulishauri acheni siasa za matusi tuwe na siasa za hoja mbadala. Tukawaambia ndani ya Bunge mjenge hoja sio kutoka nje, lakini hawakushaurika.”

Haya yanajiri siku tatu baada ya “swahiba mkuu wa Mgeja,” waziri mkuu aliyejiulu, Edward Lowassa, kutangaza kuondoka Chadema na kurejea CCM.

Mgeja ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, alijiondoa chama hicho Juni mwaka 2015 na kujiunga na Chadema ili kumfuata Lowassa katika kile walichokiita, “Alipo Tupo.”

Amesema, “…baada ya kutafakari hayo, nikaona nichukue maamuzi ya haraka maana watu tunawashauri kwa nia njema, lakini hawashauriki. Hii ni kwa sababu, ndani ya kile chama kuna ubinafsi mkubwa.”

Amesema, hakuna sababu za yeye kukaa Chadema kwa sasa, kutokana madai kuwa alichokuwa anakipigania ndani ya Chadema, kinashughulikiwa kwa kasi na Rais John Magufuli.

“Kulikuwa na sababu za msingi, zilizonifanya mimi kuondoka CCM na kwenda Chadema. Lakini kwa sasa, sababu hizo hazipo; tulichokuwa tunakipigania kinashughulikiwa na Rais Magufuli,” ameeleza Mgeja.

Amesema, “hivyo basi, leo hii, mbele yenu, nimeona nichukue maamuzi ya kuondoka Chadema na sitawaunga tena mkono maana zile sababu tulizokuwa tukizisema zinafanywa na Rais Magufuli tena kwa kasi.”

Hata hivyo, Mgeja hakueleza kwa nini ameamua kurejea kwenye siasa, wakati tayari alishautangaza kuwa amestaafu na sasa anaendelea na shughuli zake za kilimo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!