February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mwalimu aliyemchapa mwanafunzi mpaka kufa ahukumiwa kunyongwa

Spread the love

MWALIMU Respicius Mtazangira amehukumiwa na Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba adhabu ya kunyongwa hadi kufa, baada ya kupatikana na hatia ya kusababisha kifo cha mwanafunzi Sperius Eradius. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mtazangira amehukumiwa leo tarehe 6 Machi 2019 huku Mahakama hiyo ikimuachia huru aliyekuwa mshtakiwa mwenza katika kesi ya mauaji ya kukusudia, Mwalimu Herieth Gerald.

Kesi hiyo ilifunguliwa mwishoni mwa mwaka jana na kusikilizwa na Jaji Lameck Mlacha ambaye leo alisoma hukumu ya kesi hiyo.

Tukio hilo lilitokea tarehe 27 Agosti 2018, ambapo marehemu Sperius aliyekuwa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta (14) alipigwa na mwalimu Mtazangira akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu Herieth.

error: Content is protected !!