Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NICOL kutoa gawio  kwa wanahisa wake
Habari Mchanganyiko

NICOL kutoa gawio  kwa wanahisa wake

Spread the love

KAMPUNI ya Uwekezaji ya NICOL imepata faida ya shilingi bilioni 3.8 baada ya kodi na imepitisha gawio kwa wanahisa wake litakalotolewa mwezi ujao. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Gawio hilo lilipitishwa siku ya Jumamosi katika maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa mwaka wa wanahisa uliofanyika kwa njia ya video kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.

Akizungumza mara baada ya mkutano huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa NICOL, Erasto Ngamilaga, alisema Mkutano Mkuu ambao umefanyika ni takwa la kisheria kwa makampuni kama hayo kufanya na wanahisa wake wote.

Alisema kwenye mkutano huo wamehudhuria wanahisa wa mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam ambapo wale wa mikoani walifuatilia mkutano huo kupitia mtandao.

Alisema kwenye mkutano huo wamepata fursa ya kuwaeleza wanahisa namna kampuni ilivyopata faida ya Sh bilioni nne kabla ya kodi na Sh bilioni 3.8 baada ya kodi.

Alisema wanahisa wamepitisha gawio la Sh 20 kwa kila hisa ambayo itaanza kulipwa 15.12.200 na kwamba ni ongezeko la gawio la Sh 17 ambalo lilishalipwa kwenye mahesabu ya mwaka 2021.

“Wanahisa wamefurahi sana kuona kampuni inafanya vizuri na sisi viongozi tumewaaahidi kuweka mikakati mizuri zaidi kuhakikisha kampuni inazidi kusonga mbele na kupata faida kubwa zaidi siku za usoni,” alisema Ngamilaga

Mwenyekiti wa Bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda, alisema kampuni hiyo imekuwa ikitoa gawio kila mwaka na aliishukuru bodi mpya kwa kuwekeza sehemu mbalimbali hasa kwenye hati fungani za serikali.

Alisema kampuni hiyo imewekeza asilimia 30 ya uwekezaji wake kwenye hati fungani na ndiyo sababu kampuni hiyo imeendelea kupata faida mwaka hadi mwaka na kuwapa gawio zuri wanahisa wake .

Alisema wanahisa wa NICOL nchi nzima wanafikia 30,000 na wamesambaza sehemu za mikutano ili kuwafikia wanachama wengi badala ya kulazimika kuja Dar es Salaam kwenye mKutano Mkuu wa mwaka.

“NICOL inapenda kuona wanahisa wake wanapata gawio kila mwaka na kweli kampuni imefanya vizuri na gawio limeongezeka kutoka Sh 17 na sasa tutalipa sh 20 kiwango ambacho kampuni zingine zimeshindwa kufikia na tunadhani mwakani tutazidi kuongez gawio kubwa zaidi kwa wanahisa wetu,” alisema

Mwanahisa Mutamwega Mugaywa, alisema anashukuru kuona kampuni ya NICOL imesimama na kuonyesha matumaini makubwa kwa wanahisa wake.

“Nifuraha kubwa kuona NICOL inabeba uchumi na nawashauri watu wengine waje wanunue hisa zao mapema NICOL kwasababu kuna faida nyingi kuwa mwanahisa wakampuni ya wazalendo,”

“Nawapongeza viongozi kwa kusimamia vizuri Kampuni na sasa tunapata gawio zuri nawashauri wengine nao wachangamkie hisa za kampuni yetu,” alisema

Mwanahisa mwingine, Suzana Masele alimongeza Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni hiyo, Dk. Gieon Kaunda kutokana na anavoisimamia kampuni hiyo na menejimenti nzima.

“Nampongeza kwani anavyoisimamia vizuri kamouni utadhani ni kampuni yake binafsi ukiangalia ilipokuwa huko nyuma ilikuwa kama imekufa lakini mwenyekiti wa sasa anajua anachofanya na tunaelekea pazuri zaidi,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

error: Content is protected !!