Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Waliokosa mikopo elimu ya juu wapewa siku 7 kukata rufaa
Elimu

Waliokosa mikopo elimu ya juu wapewa siku 7 kukata rufaa

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru
Spread the love

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imefungua dirisha la rufaa ndani ya siku saba kwa wanafunzi ambao hawakuridhika na viwango vya mikopo walivyopata. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tangazo hilo limetolewa leo kwa vyombo vya habari ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema dirisha hilo la rufaa litakuwa wazi kwa siku saba kuanzia leo, Novemba 13 hadi 20 mwaka huu.
Amefafanua kwa rufaa kutoka kwa wanafunzi zinapaswa kuwasilishwa kwa njia ya mtandao.

“Hadi leo Novemba 13, 2022, tumeshawapangia mikopo wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 68,422 na tunafahamu kuwa kuna wanafunzi ambao kwa sababu mbalimbali, hawakukamilisha nyaraka muhimu kuthibitisha uhitaji wao, dirisha la rufaa ni fursa kwao,” amesema Badru.

Kwa mujibu wa Badru, lengo ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wapya 71,000 katika mwaka wa masomo 2022/2023 na kuwasihi wanafunzi wanaowasilisha rufaa kusoma na kuzingatia maelekezo yaliyopo kwenye mfumo wa kuwasilisha rufaa.

Kuhusu malipo, Badru amesema HESLB fedha zilianza kutumwa vyuoni hata kabla ya wanafunzi kufika vyuoni na kuwa kazi hiyo ni endelevu na kuwashauri wanafunzi waliopangiwa mikopo kufika kwa maafisa mikopo wa vyuo vyao ili kukamilisha taratibu za kupokea fedha.

“Pale mwanafunzi anapoona amepangiwa mkopo kupitia yake ya SIPA (Student’s Individual Permanent Account), basi afike kwa afisa mikopo wa chuo chake ambaye yupo palepale chuoni ili awasilishe taarifa zake za benki na kupokea fedha,” amesema Badru.

Wakati huohuo, Badru amezishukuru taasisi za elimu ya juu na serikali za wanafunzi kwa ushirikiano wanaoipatia HESLB ambao umeendelea kuimarisha ufanisi katika kuwahudumia wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu inayotolewa na Serikali kupitia HESLB.

“Kwenye huu mnyororo wa kuwahudumia wanafunzi, uongozi wa vyuo, serikali za wanafunzi na jumuiya yao ya TAHLISO ni wadau muhimu … na wamekuwa wakitupatia ushirikiano mkubwa, tunawashukuru sana,” amesema Badru.

HESLB ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na majukumu makuu mawili, kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji wa elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva ambayo imetolewa na serikali kutoka mwaka 1994/1995.

1 Comment

  • Nawapongeza sana board ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu (HESLB) kwa utendaji kazi wenu makini. But Nafikilia ni vipi continuous students tutasaidiwa ktk suala la kupangiwa mikopo? Maana naona kama tumetengwa kwa kiasi kikubwa badalaake wanatazamiwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!