Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NHIF yazidiwa, yalipa malipo kwa vituo hewa
Habari Mchanganyiko

NHIF yazidiwa, yalipa malipo kwa vituo hewa

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga
Spread the love

 

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kicheere amesema ukaguzi wa mfumo wa ulipaji wa Mfuko wa Bima ya Afya kwa watoa huduma ulibaini madai yasiyostahili kwa vituo vya huduma ya afya toka mwaka 2019 hadi 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Alibainisha hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu kwa mwaka 2021/22 kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Alisema mfuko ulilipa madai yasiyostahili tangu ta Sh 10.3 bilioni kwa vituo binafsi, Sh 1.58 kwa vituo vya Serikali na Sh 2.49 kwa vituo vya taasisi za kidini.

“NHIF ililipa madai kwa vituo vya afya visivyostahili baada ya kugundua tatizo hilo ni vituo vichache vilirejesha baadhi ya fedha na Sh 7 bilioni hazikurejeshwa na hakuna hatua iliyochukuliwa kwa watumishi walihusika,” alisema Kicheere.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere

Katika hatua nyingine CAG Kichere alisema ukaguzi umebaini kuwa matumizi kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya yamekuwa makubwa ikilinganishwa na michango yao.

Katika mwaka 2021/2022 mfuko umepata hasara ya Sh189.65 bilioni ikilinganishwa na Sh93.6 bilioni iliyokuwapo mwaka uliotangulia.

“Pia mfuko umekuwa na mtiririko hasi wa fedha katika shughuli zake za uendeshaji, mwenendo huu unaonyesha kuwa michango inaongezeka kwa asilimia 12.9 wakati matumizi yanaongezeka kwa asilimia 24.6 mara mbili,” alisema Kichere.

Alisema makadirio ya uwezo wa mfuko kujiendesha kwa Juni 30, 2021 unaonyesha kuwa mapato ya mfuko yataendelea kuwa chini ya matumizi kwa siku zijazo na mfuko utatumia ziada iliyokusanywa jambo ambalo litasababisha ukwasi kuwa hasi ifikapo mwaka 2025.

“Napendekeza kufanyiwa kazi kwa mapendekezo ya ripoti ya wataalamu na kutekeleza yaliyohitajika ili kurekebisha nakisi kama vile kuimarisha usimamizi wa utoaji huduma za afya,” alisema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!