Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Marekani yatia mguu maaandamano Kenya, yatoa maagizo kwa Rais Ruto, Odinga
Kimataifa

Marekani yatia mguu maaandamano Kenya, yatoa maagizo kwa Rais Ruto, Odinga

Spread the love

 

Mabalozi kutoka nchi sita za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, zimeonesha wasiwasi kuhusu maandamano yanayoendelea nchini Kenya na kutaka kuwepo kwa maridhiano kati ya Rais William Ruto na Kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga.

Wito huo umetolewa ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Umoja wa Afrika kutoa wito kama huo mapema wiki hii baada ya maandamano ya Jumatatu. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Hayo yamejiri wakati leo Alhamisi tarege 30 Machi 2023 maandamano yakiendelea huku kukiwa na taarifa za vurugu na uharibifu wa mali, ambao umekuwa ukishuhudiwa wakati wa maandamano hayo.

Aidha, Mabalozi hao wamepongeza hatua ya polisi nchini humo kusema kuwa, itachunguza waliovamia shamba la rais wa zamani Uhuru Kenyatta na kampuni ya Odinga wakati wa maandamano ya Jumatatu.

Odinga licha ya kukutana na kufanya mazungumzo na Seneta wa Marekani, Chris Coons pamoja na Masskofu wa Kanisa Katoliki hapo jana Jumatano amesema maandamano ya leo yataendelea, kushinikiza kushuka kwa gharama ya maisha na kudai kile anachosema haki ya uchaguzi wa mwaka uliopita.

Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Vedant Patel amevihimiza vyombo vya usalama kujizuia wakati wanapotekeleza majukumu ya kuwalinda raia na mali.

Mtaalama wa masuala ya usalama akiwa nchini Kenya, George Musamali akizungumzia wito huo wa Marekani amesema; “Marekani wanauwezo wa kupata taarifa za awali kwa sababu kuna wajasusi wengi sana wa Marekani katika mataifa ya bara Afrika haswa Kenya kwa sababu kuna masilahi yao mengi haswa nchini Kenya,”ameeleza Musamali.
Rais William Ruto ambaye anazuru Ubelgiji amekuwa akilaani maandamano ya upinzani yaliyoharamishwa na polisi na kutaka kila mmoja kuuta sheria nchini humo.

Maandamano haya ya upinzani yamesababisha baadhi ya shule nchini humo hasa jijini Nairobi kufungwa na wanafunzi kusalia nyumbani kwa kuhofia usalama wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!