SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameishauri Serikali ifanye marekebisho ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), ili itoe huduma kwa wanafunzi wa vyuo vya kati na ufundi stadi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Spika Ndugai ametoa wito huo leo Jumanne, tarehe 11 Mei 2021, jijini Dosoma, katika kilele cha mashindano ya kitaifa ya sayansi, teknolojia na ubunifu, yaliyohusisha wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati pamoja na shule za msingi na sekondari.
“Serikali iangalie ule mfuko unaosaidi wanafunzi wa elimu ya juu, sheria yake tuiangalie upya Serikali na Bunge ili badala kuangalia elimu ya juu pekee yake tuangalie wananfunzi wa vyuo vya kati vinavyotawaliwa na NACTE na VETA ili wanaofanya sayansi na teknolojia katika maeneo hayo waweze nufaika na mikopo badala ya wanafunzi wa vyuo pekee yake,” amesema Spika Ndugai.
Pia, Spika Ndugai amesema, mabadiliko hayo yawezeshe uwiano wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi na sanaa.

“Tuweke uwiano wa wanafunzi, tuiwekee msisitizo bodi yetu ya mikopo ya elimu juu ili asilimia 60 hadi 70 iende kwa wanafunzi wa sayansi na asilimis 40 iende kwa wengine. Ni wakati wa kubadili ratio (uwiano) ya mikopo inavyoenda,” amesema Spika Ndugai.
Wakati huo huo, Spika Ndugai ameshauri taasisi zinazofanya utafiti, ziongeze nguvu katika tafiti zinazohusiana na ukuaji wa uchumi wa wananchi.
“Watafiti nchini ikiwemo wa mazao ya kilimo wajitahidi kufanya tafiti zinazohusiana na ukuaji uchumi wa nchi yetu, uwafikie walengwa. Kwa kupitia tafiti hizo itasaida kusonga mbele, tuwe na tafiti nyingi zinazohusiana na maendeleo ya wananchi,” amesema Spika Ndugai.
Leave a comment