May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yaanza kukamilisha mfumo wa gesi asilia

Moja ya kituo cha gesi asilia

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, kupitia Shirika la Petroli Tanzania (TPDC) linaendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika mikoa mbalimbali. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 11 Mei, 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Steven Byabato, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Malapo.

“Je, ni lini serikali itaunganisha mfumo wa gesi asilia, kwa ajili ya kupata nishati ya kukaangia samaki katika soko la feri katika Manispaa ya Mtwara Mikindani?” ameuliza Malapo.

Byabato amejibu, Serikali inaendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia katika mkoa wa Mtwara kwa ajili ya matumizi ya viwandani, majumbani na taasisi za umma na binafsi.

Amesema, katika mkoa wa Mtwara, mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya kusambaza gesi asilia, kwa njia ya mabomba na vituo vya kuongeza mgandamizo wa gesi (Compressed Natural Gas (CNG) Station).

“Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia katika soko la feri, Manispaa ya Mtwara Mikindani, upo katika hatua ya kukamilisha usanifu wa kina wa kihandisi, utakaofuatiwa na hatua ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo.

“Kazi ya usanifu inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2021, na ujenzi kuanza Desemba 2021, na kukamilika Juni 2022, gharama za mradi huu ni takribani Sh. 10.11 bilioni,” amesema Byabato.

error: Content is protected !!