September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Ndemla atua Mtibwa, Shikalo akitambulishwa KMC

Spread the love

 

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara 2020/21, Simba ya jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, imemtoa kwa mkopo wa mwaka mmoja kiungo wake mkabaji, Said Ndemla kwenda timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro. Anaripoti Damas Ndelema…(endelea).

Leo Jumamosi, tarehe 4 Septemba 2021, ukurasa wa Twitter wa Mtibwa Sugar umeweka picha za Ndemla akisaini mkabata wa kujiunga nao na kusema “tumefanikiwa kupata saini ya kiungo fundi mwenye hadhi ya juu kabisa nchini Said Ndemla kutoka Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja.”

“Karibu sana Ndemla ufundi wako ukichanganywa na sukari yetu bora kabisa mambo yote yatakuwa,” imeeleza Mtibwa

Farouk Shikalo, Mlinda mlango mpya wa KMC

Wakati Ndemla, kiungo anayesifika kwa mashuti makali akitua kwa wakata miwa wa turiani, aliyekuwa kipa wa mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga ya Dar es Salaam, Farouk Shikalo ametambulishwa na vijana wa Kinondoni, (KMC).

Farouk ambaye ni raia wa Kenya amejiunga na KMC baada ya mkataba wake wa miaka miwili ndani ya Yanga kumalizika.

error: Content is protected !!