Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Vijana Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa za tehama
Habari Mchanganyiko

Vijana Tanzania watakiwa kuchangamkia fursa za tehama

Spread the love

 

WIZARA ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini Tanzania, imewataka vijana kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano kwa maslahi mapana ya nchi ikiwemo kutafuta fursa mbalimbali za kiuchumi na taarifa sahihi za biashara, elimu na afya. Anaripoti Vicktoria Mwakisimba, TUDARCo…(endelea).

Wito huo umetolewa jana Ijumaa, tarehe 3 Septemba 2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Zainabu Chaula wakati anazindua program ya mafunzo ya siku nane ya kampuni ya vifaa mbalimbali vya mawasiliano Huawei nchini Tanzania iitwayo ‘Seeds for the Future.’

Dk. Zainabu alisema programu hiyo ambayo itahusisha vijana 50 ni fursa nzuri na ya kipekee kwa vijana watakaopata nafasi ya kujifunza kuongeza ujuzi na uelewa wao juu ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) kisha kuwaletea faida wao binafsi na taifa kwa ujumla.

Pia, alisema katika kipindi hiki ulimwengu umeendelea na kusababisha fursa nyingi kupatikana kwa njia ya kiteknolojia ya kisasa.

Alisema katika vijana 50 vijana 40 ni wakike hali inayotia hamasa zaidi ikizingatiwa ushuhuda wa mmoja kati ya wanufaika, Emilina Masanja kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye anasema kupitia Tehama amekuza biashara yake kwa kuongeza wateja ndani na nje ya nchi.

Dk. Zainabu Chaula, Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Naye Henry Materu, miongoni mwa vijana 10 waliochaguliwa kujiunga na programu hiyo, alisema mategemeo makubwa ya mafunzo hayo ni kuleta maendeleo chanya katika sekta ya teknolojia na mawasiliano hapa nchini.

Kwa upande wake, Profesa Albino Tenge, kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma alisema chuo hicho kina tawi ambalo linafundisha teknolojia ya habari na mawasiliano inayoitwa CIVE hivyo mafunzo hayo yanatoa hamasa zaidi kwa vijana wanaosoma kozi ya Tehama.

Aidha, Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Huawei nchini, Tom Tao alisema mafunzo hayo yalianza kutolewa mwaka 2016 kwa kuchagua wanafunzi 10 wa Tehama wanaofanya vizuri kutoka katika taasisi za elimu ya juu, kutokana na mlipuko wa Uviko 19 kuanzia mwaka jana mafunzo hayo yamekuwa yakitolewa kwa mjia ya mtandao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!