May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndayiragije aibukia Geita Gold

Etienne Ndayiragije, Kocha wa Taifa Stars

Spread the love

 

KLABU ya Geita Gold imemtangza rasmi aliyekuwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Etienne Ndayilagije kuwa kocha mkuu wa kikosi hiko mara baada ya kusaini mkataba. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Klabu hiyo itacheza Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa mara ya kwanza kwenye msimu ujao, toka ilipopanda daraja kwenye Ligi Kuu, ikitoka Ligi daraja la kwanza kwenye msimu wa 2020/21.

Geita Gold iolimtangaza kocha huyo, kupitia kurasa zao za kwenye mitandao ya kijamii, bila kueleza ni mkataba wa muda gani.

Ndayiragije ambaye ni raia wa Burundi anarejea tena nchini Tanzania mara baada ya kutimuliwa kama kocha mkuu kwenye kikosi cha Taifa Stars Februari, mwaka huu kufuatia kupata matokeo mabovu kwenye michuano ya kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) iliyofanyika nchini Cameroon, mwaka jana.

Hii itakuwa klabu yake ya nne kufundisha ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kufuatia kuzinoa klabu kama Mbao Fc, Kmc na Azam FC

error: Content is protected !!