May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Soufiane Rahimin abeba ndoo, aaga rasmi

Spread the love

 

Mshambuliaji nyota wa Klabu ya Raja Club Athletic kutoka nchini Morocco, Soufiane Rahimi jana tarehe 21 Agosti, 2021 ameisaidia timu yake kutwaa kombe la Mfalme Mohammed VI na kutumia mchezo huo kuwaaga mashabiki wa timu hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Katika mchezo huo ambao Raja walikuwa wakipepetana na Saudi Al Ittihad ya Saudi Arabia, walitoka sare ya bao 4-4 katika dakika 90, kisha wakaenda kwenye penalti ambapo Raja waliibuka washindi kwa penalti 4-3.

Rahimi ambaye anatarajiwa kuelekea kwa mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya nchini Misri, aliifungia timu yake mara mbili.

Baada mchezo huo aliomba msamaha kwa mashabiki wa Raja kwa kuondoka klabuni.

Baba Rahimi ambaye ni msimamizi wa vifaa vya klabu anayeonekana pichani akilia baada ya mwanae kuaga.

error: Content is protected !!