Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Rais Samia apokea kombe la CECAFA, ataka bursa itumike michuano kombe la Dunia
Michezo

Rais Samia apokea kombe la CECAFA, ataka bursa itumike michuano kombe la Dunia

Rais Samia Suluhu Hassan (kushoto) akishuhudia mchezo kati ya Simba na Yanga
Spread the love

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amewataka wafanya biashara nchini pamoja na sekta binafsi nchini, kuchangamkia fursa kwenye michuano ya kombe Dunia 2022, itakayofanyika Qatar. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Samia ameyasema hayo leo jumapili Agosti 22, Ikulu jijini Dar es Salaam, kwenye hafla ya kupokea kombe la ubingwa wa CECAFA, kwa Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23.

Katika hafla hiyo ambayo iliudhuliwa na wachezaji wa Timu ya Taifa ya vijana, pamoja na wageni mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Innocent Bashungwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia.

Kuelekea kwenye michuano hiyo, Mwakani Rais Samia aliwataka wafanya biashara kuangalia fursa mbalimbali zitakazopatikana nchini Qatar ili zinufaishe nchi.

“Kama mnavyofahamu mwakani kutakuwa na mashindao ya kombe la Dunia Qatar, na hapa na Qatar sio mbali, natoa wito kwa wafanyabiashara nchini kuangalia fursa ambazo tutanufaika nazo kama nchi.” alisema  Rais Samia

Aidha Rais Samia aliwapongeza alipongeza timu hiyo ya vijana kwa kufanikisha kutwaa taji hilo na kusema kuwa taji hilo, litakuwa chachu na mwanzo wa kushinda makombe mengine.

“Wakati nikihutubia Bunge mwezi April Mwaka huu, nilisema serikali itakuza michezo nchini na leo ninafuraha kupokea kombe hili la ubingwa Afrika Mashariki na amini hii itakuwa mwanzo wa Safari wa kwenda kuchukua makombe mengine.” Alisema Rais Samia

Timu hiyo ya Taifa ya vijana ilishinda kombe hilo Julai 30, mwaka huu nchini Burundi kwa kuwafunga wenyeji kwenye mchezo wa fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penati 6-5.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!