Monday , 5 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NCCR- Mageuzi yafanya mabadiliko ya uongozi
Habari za SiasaTangulizi

NCCR- Mageuzi yafanya mabadiliko ya uongozi

James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi
Spread the love

CHAMA cha NCCR- Magezi, nchini Tanzania, kimefanya mabadiliko makubwa katika uongozi wake wa kitaifa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika mabadiliko hayo, Martha Chiomba, ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Kawe, kwenye uchaguzi mkuu uliyopita, amepitishwa kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho.

Chiomba ambaye alitikisa kampeni za uchaguzi katika jimbo la Kawe, kutokana na staili yake ya kampeni za “nyumba kwa nyumba,” amechukua nafasi hiyo, kutoka kwa Elizabeth Mhagama.

Taarifa zinasema, Elizabeth amefikia maamuzi ya kujiuzulu wadhifa huo, kutokana na kutingwa na majukumu yake binafsi na yale ya familia.

Martha Chiomba

Elizabeth Martin Mhagama, ni wakili wa kujitegemea, anayeyefanyia shughuli zake jijini Dar es Salaam, ambaye amejikita katika sheria za ajira. Alipata shahada yake ya sheria, katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Kabla ya kuwa katibu mkuu, Elizabethi amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho, ikiwamo afisa wa Idara ya Katiba na Sheria, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Naibu Katibu Mkuu (Bara).

Naye aliyekuwa mbunge wa Moshi Vijijini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Anthony Calist Komu, amechaguliwa kuwa naibu katibu mkuu mpya wa chama hicho, Tanzania Bara.

Komu, alikuwa mmoja wa wasisi wa NCCR – Mageuzi, amechukua nafasi hiyo, kutoka kwa Rehema Sam Kahangwa.

Mwanasiasa huyo machachari alijiunga na NCCR- Mageuzi, wakati kikiwa vuguvugu la kudai kuwapo mfumo wa vyama vingi nchini – The National Convention for Construction and Reform – mwaka 1990.

Wakati Komu anaendesha vuguvugu hilo, alikuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mbunge wa Moshi Vijijini Anthony Komu

Mwingine aliyechaguliwa katika uongozi huo mpya, ni Suzana Maselle, ambaye alijiunga na chama hicho, kutokea Chadema, ambako alikuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri kati ya Novemba mwaka 2015 na Julai mwaka 2020.

Katika hatua nyingine, NCCR- Mageuzi kimerejesha upya mamlaka ya Kamati Kuu (CC), ambayo yalikuwa yameondolewa huko nyuma.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, mabadiliko haya, tayasaidia sana chama hicho, kujisuka upya na kurejesha heshima yake ambayo ilitoweka kufuatia kuibuka kwa mgogoro mkubwa wa uongozi kati ya aliyekuwa mwenyekiti wake, Augustine Mrema na katibu mkuu wake, Mabere Marando.

Katika mgogoro huo, Mrema alidai kuwa Marando na Kamati Kuu (CC), wanataka kumuondoa kwenye kiti chake na hivyo akapendekeza kwa NEC, kumfukuza Marando, kuvunja CC na kuwafuta uwanachama viongozi wengine wandamizi, jaribio ambalo lilishindwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

error: Content is protected !!