Saturday , 15 June 2024
Home Habari Mchanganyiko NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake
Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM za NBC inayolenga kuwapa watumiaji wake nafasi ya kujishindia zawadi na kuwa sehemu ya kufurahia udhamini wa benki hiyo kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Zawadi za kusisimua, ikiwa ni pamoja na tiketi za kushuhudia mechi za Ligi kuu ya Mabingwa ya NBC, jezi, na zawadi nyingine kemkem zinatarajiwa kushindaniwa.

Meneja wa Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Lilian Mutalemwa akitoa zawadi ya Jezi kwa mmoja wa washindi wa Kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC Dosian Augustine baada ya kushinda alipofanya muamala wake katika mashine ya ATM .

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika Tawi Benki la NBC la Mlimani City jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC, David Raymond alisema Kampeni hiyo inalenga kuhamasisha wateja wa NBC na wasio wateja wa benki hiyo kutumia mashine za ATM za NBC kufanya miamala yao.

Amesema wateja ambao watatumia kadi zao za ATM kufanya miamala mbalimbali katika kipindi cha kampeni watapata nafasi ya kushinda zawadi za kusisimua, ikiwa ni pamoja na tiketi za kushuhudia Ligi ya Mabingwa ya NBC, Jezi, na zawadi nyingine kemkem.

“Tunayo furaha kuzindua kampeni hii ya mkeka wa ushindi na ATM za NBC ambayo inawazawadia watumiaji wote wa ATM za NBC ikiwa ni wateja wa NBC na wasio wateja wa NBC.

“Tunaelewa umuhimu wa urahisi katika huduma za benki, tunazidi kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja kwa kuongeza ATM mpya kwenye maeneo mbalimbali nchini. Watumiaji wa ATM za NBC wanaweza kuweka pesa kwenye akaunti yoyote ya NBC kupitia ATM zilizopo kwenye matawi yetu nchi nzima,” amesema David.

Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC, David Raymond, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC zilzofanyika mapema leo katika tawi la Mlimani city.

Ameongeza “Pia wale wasiokuwa na akaunti yoyote wanaotumiwa fedha kwa kutumia huduma ya NBC taslimu popote, wanaweza kutoa pesa hizo kwenye ATM yoyote ya NBC. Wote walio na kadi za VISA, Union Pay na Mastercard wanaweza kutumia ATM za NBC kutoa pesa.

“Makundi yote haya yanayo nafasi sawa ya kujishindia zawadi hizi katika kampeni hii. Tunaamini kuwa watumiaji wa ATM za NBC wataendelea kufurahia huduma zetu, tunawakaribisha wote watumie ATM za NBC,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias ameongeza kuwa zawadi hizo zitakuwa ni za papo kwa papo, pale mteja akifanya muamala wake kwa kutumia ATM ya NBC atapata kujua kuwa ameshinda zawadi gani kwa kuangalia nyuma ya risiti ya muamala wake.

“Sisi kama benki ya NBC, daima tunawaweka wateja wetu karibu na kuhakikisha wanafurahia huduma zetu wakati wowote na popote. Kampeni yetu ya mkeka wa ushindi na ATM za NBC tunafurahi kuwapa  wateja wetu nafasi ya kushinda tiketi za kuona Ligi ya Mabingwa, jezi, na vitu vingine vya kumbukumbu ya Ligi ya NBC.

“Tunatumaini kuwa kampeni hii itaimarisha zaidi uhusiano wetu na wateja wetu pamoja na watumiaji wote wa ATM zetu.” amesema Urlik

Amesema kampeni hiyo inawalenga watumiaji wote wa ATM za Benki ya NBC za Dar es Salaam na Kibaha.

“Kila mtumiaji wa ATM za NBC akishafanya muamala, achukue risiti yake, aigeuze nyuma kuangalia zawadi aliyoshinda. Kisha aende na risiti yake kwenye tawi lolote lililo karibu naye ili kuchukua zawadi yake,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Rais Samia amng’oa Matinyi Serikalini, ateua viongozi mbalimbali

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali akiwamo...

Habari Mchanganyiko

DAWASA yaja na suluhisho la maji kwa wakazi wa Sinza C,D

Spread the loveWakazi wa Kata ya Sinza, Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Samia: Wakuu wa mikoa, wilaya wanaendeleza ubabe

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema bado wakuu wa wilaya na...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Vitalu 19 vya madini vyazalisha ajira 12,000 Songwe

Spread the loveZAIDI ya vijana 12,000 kutoka Wilaya ya Songwe mkoani Songwe...

error: Content is protected !!