Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari Nape: Nimerudi kusimamia sheria ya habari
Habari

Nape: Nimerudi kusimamia sheria ya habari

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Spread the love

 

WAZIRI wa Habari, Nape Nnauye, amesema amerudi katika wizara hiyo, ili kusimamia Sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari ya 2016, aliyosimamia utungwaji wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Nape ametoa kauli hiyo leo Jumatano, tarehe 12 Januari 2022, jijini Mwanza, katika shughuli ya kuiaga miili ya wanahabari watano, waliofariki dunia jana Jumanne, katika ajali iliyotokea mkoani Simiyu.

Mbunge huyo wa Mtama (CCM), amerudishwa katika wizara hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan, tarehe 8 Januari mwaka 2022, ikiwa ni takibani miaka mitano tangu aondolewe kwenye wadhifa huo na Hayati John Magufuli, Machi 2017.

Nape amesema amerudi kusimamia utekelezwaji wa sheria hiyo, baada ya kusuasua kwa muda.

“Najua katikati kulikuwa na kusuasua kutekeleza sheria hii, nataka niwahakikishie wanahabari nimerudi nyumbani kuishughulikia sheria hii. Nataka niwahakikishie nimerudi nyumbani kuishughulikia na tutaitekeleza haki zenu zitalidnwa,” amesema Nape.

Aidha, Nape amesema Rais Samia Suluhu Hassan, ameagiza sheria hiyo ifanyie marekebisho, ili kuondoa mapungufu yake.

“Sababu ilitungwa na binadamu inawezekana yako mapungufu ya hapa na pale. Rais ameshaagiza tutayapitia mapungufu hayo, tutayarekebisha na kuhakikisha yanakidhi matarajiao na yale ambayo wanahabari wanayataka kwenye sheria hiyo,” amesema Nape.

Nape amewahakikishia wanahabari kuwa, Serikali ya Rais Samia itawatengenezea mazingira mazuri na salama ya utendaji kazi wao.

“Kazi ya Seriikali ni kuhakikisha tunawtengenezea mazingira mazuri ya ninyi kufanya kazi, niwahakikishieni uhuru wenu, haki zenu ziko salama chini ya mikono ya Rais Samia na mimi kama muwakilishi wake nitasimamia na tunaanzia hapa leo,” amesema Nape.

Nape ametoa kauli hiyo baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan, kuomba kuzungumza naye juu ya namna ya kupata sheria nzuri zitakazotatua matatizo ya waandishi wa habari, ikiwemo maslahi yao.

Nape aliondolewa katika nafasi ya uwaziri wa habari na Hayati Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano.

Siku moja baada ya kukabidhi ripoti ya tume aliyoiunda kuchunguza tukio la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuvamia Kituo cha Televisheni cha Clouds (Clouds Media ).

Katika ripoti hiyo, ilionesha Makonda alivamia kituo hicho, usiku wa tarehe 17 Machi 2017.

Wanahabari waliopoteza maisha ajalini wakiwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel jana Jumanne wakienda Ukerewe mkoani Mwanza, ni Abel Ngapemba (aliyekuwa Afisa Habari Mkoa wa Mwanza), Johari Shani (Uhuru Digital) ambaye pia ni askari polisi.

Wengine ni, Husna Mlanzi (ITV), Steven Msengi (Afisa Habari Ukerewe) na Antony Chuwa (Habari Leo Online)

Miili ya marehemu imesafirishwa kwenda kuzikwa mikoani kwao huku mwili wa Husna unazikwa leo jijini Mwanza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!