Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Nape ashauri Mdee na wenzake wafukuzwe bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Nape ashauri Mdee na wenzake wafukuzwe bungeni

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Spread the love

 

MBUNGE wa Mtama (CCM), Nape Nnauye, ameshauri wabunge viti maalum 19, waliovuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waondolewe bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Nape ametoa ushauri huo jana tarehe 23 Aprili 2021, katika mjadala wa haki za vyama vya siasa uliofanyika mtandaoni, baada ya kuulizwa maoni yake kuhusu sakata hilo la Mdee na wenzake kufukuzwa Chadema.

Wabunge hao waliofukuzwa Chadema Novemba 2020 kwa tuhuma za usaliti ni, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee. Waliokuwa Wajumbe wa Kamati Kuu wa chama hicho, Ester Bulaya na Esther Matiko.

Wengine ni, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga, Agnesta Lambart, Asia Mohamed, Nusrat Hanje, Tunza Malapo, Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda , Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

Akizungumzia sakata hilo, Nape amehoji “katiba inasema hatuwezi kuwa na watu ambao hawana vyama, Sasa kama mifumo inasita, then kuna hatua za kuchukua kufuata maamuzi sahihi ya vyama vyao.

Hili liko wazi, nadhani kama hawa wanasema wanachama wa chama fulani, chama hicho kinasema hawa si wanachama wetu, then mnabaki nao vipi?”

Mwanasiasa huyo ameshauri maamuzi ya Chadema ya kuwafukuza uanachama wabunge hao yaheshimiwe.

“Kwa mtazamo wangu nadhani tuheshimu tasisi zinazotengeneza demokrasia, taasisi hizo pamoja na vyama vya siasa. Kama wameamua kuwafukuza wanachama wao, mi andhani ni muhimu hili jambo lingeheshimiwa kwamba wamefukuza wananchama wao,” amese

1 Comment

  • Asante nape ukweli usemwe mnyonge kabla hamjanyonga mpeni haki yake kwanza alafu ndio anyongwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!