May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaishusha Yanga kileleni

Spread the love

Bao la dakika ya 28 lililofungwa na Mohammed Hussein kwenye mchezo dhidi ya Gwambina lilitosha kuipeleka Simba kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuishusha Yanga. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Mchezo huo ulipigwa hii leo kwenye Uwanja wa Gwambina uliopo Misumbwi mkoani Mwanza.

Mechi hiyo ilikuwa yenye mvuto wa aina yake kutokana timu zote kucheza na taadhari kubwa kutokana na ubora wa vikosi vya timu zote mbili.

Iliwachukua Simba dakika 28 kwa Simba kuandika bao hilo la kwanza na la ushindi lililofungwa kwa shuti kali na beki wa kushoto wa Simba Mohamed Hussen na kudumu mpaka dakika 90 ya mchezo.

Matokeo ya mchezo huo yaliifanya Simba kuishusha Yanga kwa tofauti ya alama moja na Simba akiwa nyuma kwa michezo miwili.

Simba inafikisha pointi 58, wakiwa na michezo 24 huku Yanga iliyoongoza Ligi hiyo muda mrefu, imepolomoka mpaka nafasi ya pili wakiwa na pointi 57 na michezo 26.

Yanga itashuka dimbani kesho kupambana na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!