May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Lissu aichambua hotuba ya Rais Samia, aibua hoja

Tundu Lissu

Spread the love

TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, amesema alitarajia kuona Rais Samia Suluhu Hassan, anatumia muda mrefu kuzungumzia mustakabali wa demokrasia na vyama vya siasa, kwenye Hotuba yake aliyoitoa bungeni jijini Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). 

Lissu amesema hayo jana tarehe 23 Aprili 2021, siku moja baada ya Rais huyo wa Awamu ya Sita, kulihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza, tangu alipoapishwa tarehe 19 Machi 2021, kuchukua mikoba ya Hayati Dk. John Magufuli, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi mwaka huu.

“Kama rais kwenye dakika 92 na sekunde 20 anatumia dakika moja na sekunde tano kutaja vyama vya siasa. Hakuna demokrasia , hakuna haki, vingine vyote hakuna, only one minute ametumia kutaja vyama vya siasa, tunaachaje kuwa na wasiwasi?” amehoji Lissu.

Mwanasiasa huyo aliyeko nchini Ubelgiji, amesema alitarajia Rais Samia aitumie hotuba hiyo kuzungumzia uhuru wa vyama vya siasa na wafungwa wa kisiasa akisema kwamba masuala hayo yako chini ya mamlaka yake.

 “ Ilikuwa si vibaya kutegemea kwamba, kwenye hotuba ya jana (Juzi Alhamisi) ya Rais Samia kuna mambo ambayo anaweza kuyafanya bila kubadilisha sheria, kusema kwamba vyama vya siasa vina uhuru kufanya shughuli zao, haihitaji mabadiliko ya sheria” amesema Lissu.

Mwanasiasa huyo amesema  “Haihitaji kubadili sheria kusema kwamba wote waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa sababu za kisiasa, waachiwe na wako wengi sisi Chadema peke yake wako zaidi ya 400, hivi tunavyozungumza.”

Lissu amesema, katika hotuba hiyo alitarajia kuona Rais Samia anazungumzia wanasiasa walioondoka nchini kwa sababu mbalimbali, akiwemo yeye.

“Haihitaji mabadiliko ya sheria kusema kwamba wale ambao wamelazimika kukimbia nchi kama mie warudi nchini tutawalinda,” amesema Lissu.

Lissu pamoja na Godbless Lema, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, waliondoka nchini baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2020, kwa madai ya kuhofia usalama wa maisha.

Hata hivyo, Insepekta Generali wa Polisi nchini (IGP), Simon Sirro aliwaita wanasiasa hao warejee nchini huku akiwahakikishia ulinzi.

Makamu mwenyekiti huyo wa Chadema Bara amesema, masuala hayo na mengine yanafanya baadhi ya watu hasa wanasiasa kuwa na shaka juu ya uongozi wake mpya.

Lissu amesema ili hofu hiyo itoweke, Rais Samia anatakiwa kufanyia kazi  changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye uongozi wa mtangulizi wake, ikiwemo kuwaacha huru wafungwa wa kisiasa, kufuta kesi za kubambikiza na kuwahakikishia ulinzi wanasiasa walioko nje ya nchi, ili warudi Tanzania.

“Ili sasa kuwe na upatanisho, kuwe na haya mambo. Kuna vitu ambavyo vinatakiwa vifanyike ili kuondoa hizi hofu na maumivu, kwa kauli tu hatujaenda. Tulitaka mama aseme hivyo, aseme kwamba wote ambao wamekimbia warudi tutawapa ulinzi,” amesema Lissu na kuongeza:

tufutiwe mashtaka ya bure ambayo tumefunguliwa, mimi nina kesi sita peke yangu. Na  wale ambao wamenyang’anywa mali zao warudishiwe.”

error: Content is protected !!