Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Nape aibua sakata la korosho, Spika Ndugai aibana Serikali
Habari za Siasa

Nape aibua sakata la korosho, Spika Ndugai aibana Serikali

Nape Nnauye, Mbunge wa Mtama (CCM)
Spread the love

 

MBUNGE wa Mtama mkoani Lindi (CCM), Nape Nnauye, ameiomba Serikali irudishe Bodi ya Korosho pamoja na fedha za tozo ya mauzo ya nje ya nchi (Export Levy), kwa wakulima wa zao hilo, ili kulinusuru lisife. Anaripoti Nasra Bakari, DMC…(endelea).

Nape alitoa ombi hilo jana tarehe 24 Mei 2021, katika mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022, bungeni jijini Dodoma.

Mwaka 2018, Serikali ya Tanzania ilifanya mabadiliko katika sheria ya taasnia ya korosho, ambayo yalisababisha fedha zote za tozo ya mauzo ya zao hilo nje ya nchi, kupelekwa katika mfuko mkuu wa fedha za Serikali, badala ya mfuko wa kuendeleza korosho.

Kufuatia mabadiliko hayo, Mbunge huyo wa Mtama ameiomba Serikali irudishe utaratibu wa zamani, wa fedha hizo kupewa wakulima kwa ajili ya kugharamia shughuli za uzalishaji wa korosho.

“Kwa mahesabu ya kawaida, 2018 iliingizwa Sh. 37 bilioni wakati mfuko ukifanya kazi ya kugharamia pembejeo, Serikali ilipata mapato Sh. 1 trilioni na zaidi, kwa kuingiza kiasi hicho cha fedha tu. Mwaka huu makisio ya uzalishaji ni tani 280,000 hadi 350,000, tunahitaji Sh. 55 bilioni tu,” alisema Nape.

Mwanasiasa huyo alisema “Maombi yangu kwa Serikali na bahati nzuri naibu waziri (Hussein Bashe), wakati ule tuna mgogoro wa tozo ya ushuru wa nje hapa bungeni. Alikuwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti na alituunga mkono,”

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

“Matumaini yangu kwenda kwake serikalini hakujambadilisha kuliona jambo hili kwa usahihi, tuchukue fedha ya export levy turudishe kugharamia korosho,” alisema Nape.

Baada ya Nape kutoa maombi hayo, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimuagiza Waziri wa Kilimo, Prof. Adolph Mkenda, atoe majibu ya kina kuhusu suala hilo, leo tarehe 25 Mei 2021, wakati anahitimisha hoja yake kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha ujao.

“Utakapohitimisha hoja yako, mambo haya na kwa msingi yalivyokuwa tungependa kusikia Serikali inasemaje,” alisema Spika Ndugai na kuongeza”

“Na kesho (leo), wakati wa mafungu nitakuwa nimekaa hapa. Wakikubana nitawaacha na nikiri kwamba, bahati mbaya na mimi ni mkulima wa korosho. Kwa hiyo kesho (leo) tunataka majibu, ili twende mbele kwenye zao la korosho.”

Katika mjadala huo, Nape alisema tangu Serikali ifanye mabadiliko ya sheria ya tasnia ya korosho mwaka 2018, yaliyosabaishwa bodi hiyo kuvunjwa, uzalishaji zao hilo ulianza kuporomoka.

“2018 tulibadilisha sheria ya tasnia ya korosho. Yale mabadiliko yalisababisha mfuko wa kuendeleza zao la korosho ambao ulikuwa unaitwa mfuko wa pembejeo, ambao chanzo chake cha fedha kilikuwa tozo ya mauzo ya nje, Serikali iliufuta, ” alisema Nape.

Mwanasiasa huyo alisema “uamuzi ule wa kuchukua fedha katika mfuko ule ulipofanyika, Serikali ilitoa ahadi kwamba zile fedha ziliopatikana, zinapelekwa katika mfuko mkuu zikasimamiwe vizuri. Kwa hoja zilipokuwa katika mfuko hazisimamiwi vizuri.”

Mbunge huyo wa Mtama alisema, badala ya jitihada za kuongeza uzalishaji wake kufanyika, Serikali imewaongezea wakulima mzigo wa tozo.

Zao la Korosho

“Baada ya fedha kuchukuliwa, korosho uzalishaji wake ukashuka kutoka tani 320,000, ukaenda tani 200,000 na kitu, kwa maamuzi ya kuchukua mfuko. Lakini mbaya zaidi badala ya kurudisha fedha kwa wakulima, kilichofanyika msimu uliofuata , Serikali ikaleta mapendekezo ya kuweka tozo kwa wakulima,” alisema Nape.

Nape alisema, katika mapendekezo hayo, Serikali ilipanga kuwatoza wakulima wa korosho Sh. 25 kwa ajili ya kugharamia utafiti na Sh. 25 kuendesha Bodi ya Korosho.

“Kwa hiyo wanakatwa Sh. 50 kwa ajili utafiti na kuendesha Bodi ya Korosho, huu ni udanganyifu. Tulipoahidiwa hapa bungeni tuliambiwa fedha ingeenda kwa wakulima, huu mzigo aliobebeshwa mkulima,” alisema Nape na kuongeza:

“Mbaya zaidi sasa hivi yapo mapendekezo mengine ya kugharamia pembejeo, kwa kumkata mkulima Sh. 110 kwa kilo. Ahadi iliyotolewa hapa bungeni, hii fedha ya export levy ingerudi kugharamia.

Kwa nini tunataka kumbebesha mzigo mkulima, badala ya kuchukua fedha ambayo mlituahidi hapa itakwenda kutumika vizuri?”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!