Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Tangulizi Wabunge walia na Wizara ya Kilimo
Tangulizi

Wabunge walia na Wizara ya Kilimo

Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu
Spread the love

 

WIZARA ya Kilimo nchini Tanzania, imeshauriwa ibadilishe utendaji wake katika kuiendeleza sekta ya kilimo, kutoka kwenye mikakati ya nadharia kwenda kwa vitendo. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Ushauri huo ulitolewa na wabunge jana tarehe 25 Mei 2021, katika mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Akizungumza katika mjadala huo, Mbunge wa Rorya mkoani Mara (CCM), Jafari Chege, aliishauri wizara hiyo ibadilishe matokeo ya tafiti zilizofanywa na wataalamu wa kilimo nchini, kutoka nadharia kuwa ya vitendo, kwa ajili ya kuimarisha sekta hiyo.

“Imani yangu mtabadilisha kilimo kutoka nadhari kwenda vitendo, kwa miaka yote toka uhuru hakuna kitu ambacho hakijaandikwa kuhusu kilimo. Kazi kwenu kutumia tafiti za wataalamu, kuondoa nadharia ya kilimo kuwa vitendo,” alisema Chege.

Mbunge Chege

Mbunge wa Urambo mkoani Tabora (CCM), Margaret Sitta, aliishauri wizara hiyo kuondoa changamoto ya masoko, pamoja na kuwahamasisha wakulima kujikita kwenye kilimo cha kisasa.

“Kuna haja gani kuwahimiza watu walime, baada ya hapo wanakosa masoko? Waziri atusaidie tunafanyaje wakulima walime, kutokana na jinsi mnavyowafundisha kilimo cha kisasa. lakini muhimu suala la mbolea kufika kwa wakati,” alisema Sitta.

Margaret Sitta

Mbunge wa Singida Mashariki (CCM), Miraji Mtaturu, aliishauri wizara hiyo ifanye marekebisho katika utendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), ili iwe rafiki kwa wakulima.

“Kuna benki hazina urafiki na wananchi wa kawaida, hata hii benki ya kilimo ambayo Serikali imeweka fedha ili tuwawekee wakulima wetu mazingira rafiki, haina urafiki na wakulima,” alisema Mtaturu.

Mtaturu alisema “haiwezekani waliopewa mkataba wa mkopo na watu wa bima wapo, mwisho wa siku wasipovuna vizuri wanapelekwa mahakamani. Huyu mkulima unamfanya aogope. Pamoja na juhudi za kuongeza fedha, kuna vitu vinafanywa havimsaidia mkulima.”

Miraji Mtaturu

Aidha, Mtaturu aliishauri wizara hiyo iongeze wataalamu wa kilimo, hasa cha umwagiliaji katika halmashauri, ili kuwasaidia wakulima.

“Kilimo cha umwagiliaji kipewe nafasi kubwa, hekta zinatengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji lakini hii haitoshi. Tuongeze wataalamu kwenye halmashauri , leo hii unaweka skimu za umwagiliaji zinakabidhiwa kwa wakulima ambao hawawezi kuendesha miradi ile, tunapoteza fedha ,” alisema Mtaturu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda kuanika mawaziri wanaomtukana Samia

Spread the loveMKUU Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka watu wanaowatuma mawakala...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yafafanua hatima ya viongozi NEC

Spread the loveWAKATI mjadala ukiibuka  juu ya hatma ya viongozi wa sasa...

error: Content is protected !!