KAMA itafanikiwa kuvuka kwenye mchezo wa pili dhidi ya Costo De Agosto ya Angola, klabu ya Namungo ya Tanzania, itaangukia kwenye kundi D ya michuano Kombe la Shiriki. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Kundi hilo, linajumuisha timu za Raja Athletic Club kutoka Morocco, Pyramid FC kutoka Misri pamoja na Nkana Red Devil ya nchini Zambia.
Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa jana Jumapili, Namungo FC alifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-2, ambao walicheza ugenini katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huo, ulichezwa Tanzania, mara badaa ya shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), kuamuru mechi zote mbili kuchezwa nchini Tanzania.

Kwa matokeo hayo, Namungo ananafasi kubwa ya kufuzu kwenye hatua ya makundi kutokana na kuwa na mtaji mkubwa wa kutosha wa mabao waliopata kwenye mchezo wa kwanza.
Makundi hayo ambayo yamepangwa leo Jumatatu, tarehe 22 Februari 2021, jijini Cairo nchini Misri na Namungo kupangwa kwenye kundi sambamba na timu mbili kutoka uarabuni ambao wanauzoefu mkubwa wa mashindano.
Raja Athelitic Club ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Morocco, walifanikiwa kucheza hatua ya nusu fainali ya kombe la Ligi ya mabingwa barani Afrika na kuondoshwa kwenye michuano hiyo na Zamalek kutoka Misri.
Kwa upande wa Pyramid FC, wanaoshiriki Ligi Kuu nchini Misri ambapo walifanikiwa kufika fainali ya michuano hiyo kwenye msimu uliopita licha ya kufungwa na klabu ya RS Berkane.

Ikumbukwe CAF, walieleza kati ya Namungo na Costo De Agosto hawatozingatiwa viwango katika hatua ya upangwaji wa makundi hayo mara baada ya kufutwa kwa mchezo wa kwanza uliopangwa kuchezwa tarehe 14 Februari 2021, nchini Angola.
Leave a comment