Spread the love

BENKI ya NMB Tanzania walikuwa ni miongoni mwa washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Wahandisi na Makandarasi wa miundombinu la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kuimarisha wakandarasi wa ndani. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Naibu Waziri wa Ujenzi na uchukuzi, Godfrey Kasekenya (kushoto) akizungumza na watumishi wa Benki ya NMB walipokutana kwenye Kongamano la Kitaifa la Wahandisi na Makandarasi wa miundombinu la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kuimarisha wakandarasi wa ndani lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni mkuu wa Idara ya Miamala wa Benki ya NMB, Linda Teggisa.

Kongamano hilo lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma ambapo Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alipata wasaaa wa kuzungumza na watumishi wa Benki ya NMB.

Tuzo hiyo ilitolewa tarehe 25 Mei 2022 katika mkutano mkuu wa mwaka wa 57 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na mambo mengine ukijadili fursa mbalimbali na changamoto zinazolikabili Bara la Afrika uliofanyika Accra nchini Ghana.

Mkuu wa Miamala Benki ya NMB Makao makuu ,Linda Teggisa akiwasilisha mada kuhusu huduma zinazotolewa na NMB kwenye Kongamano la Kitaifa la Wahandisi na Wakandarasi wa miundombinu la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake katika kuimarisha wakandarasi wa ndani lililofanyika mwisho wa wiki ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. NMB walidhamini Kongamano hilo.

Tuzi hiyo ni ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) ikiwa ni kutambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu nchini ambapo Rais Samia aliipokea mwenyewe kutoka kwa Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Solomon Quaynor kwa niaba ya Rais wa Benki hiyo, Dk Akinumwi Adesina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *