August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serengeti Girls yatinga bungeni, Nahodha ahutubia

Spread the love

 

NI heshima kubwa. Ndivyo unaweza kuelezea kile ambacho Timu ya Taifa ya soka la Wanawake chini ya miaka 17 ‘Serengeti Girls’ ya Tanzania imekipata kwa Bunge la Taifa hilo kuingia ndani ya ukumbi wa Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Timu hiyo ya benchi la ufundi na viongozi wa wizara ya utamaduni, sanaa na michezo na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo Jumanne, tarehe 7 Juni 2022 wamepewa heshima hiyo na muhimili huo nyeti nchini humo.

Hiyo ni kutokana na mafanikio waliyoyapata ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia nchini India Oktoba 2022 kwa kuwaondoa Cameroon kwa jumla ya magoli 5-1.

Kabla ya timu hiyo kuingia bungeni, kanuni za Bunge zilitenguliwa ili kuruhusu kuingia ukumbini na kupata fursa ya kukaa viti vya wabunge na nahodha wa timu hiyo kulihutubia Bunge hilo.

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amewapongeza na kuwataka kwenda kuiwakilisha vyema nchi na kuhakikisha wanarudi na Kombe la Dunia.

error: Content is protected !!