Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Mwijaku kizimbani tuhuma za kusambaza picha za ngono
Habari Mchanganyiko

Mwijaku kizimbani tuhuma za kusambaza picha za ngono

Msanii wa uigizaji nchini Tanzania, Mwemba Burton (35) 'Mwijaku'
Spread the love

MSANII wa uigizaji nchini Tanzania, Mwemba Burton (35) maarufu Mwijaku amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akituhumiwa kusambaza picha za ngon kinyume cha sheria. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Leo Jumatano tarehe 29 Julai 2020, Mwijaku amesomewa shtaki moja na Wakili wa Serikali Mkuu, Simon Wankyo akisaidiwa na Mwanamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

Wakili Mwamina amemsomea shtaka linalomkabili mtuhumiwa huyo ambalo ni kusambaza picha za utupu.

Inadaiwa kati ya tarehe 17 Septemba 2019 na tarehe 10 Oktoba 2019, kwa kutumia mtandao wa WhatsApp alisambaza picha za ngono.

Baada ya kusomewa shtakiwa hilo, mshtakiwa amekana shtaka hilo.

Wakili Wanyko ameiambia mahakama hiyo, upelelezi wa shauri hilo unaelekea ukingoni.

“Sehemu kubwa ya upelelezi umekamilika, imebakia sehemu ndogo tunaomba ipangawe tarehe nyengine,” amesema

Wankyo ameiomba Mahakama hiyo kumpa masharti ya dhamana yatakayomfanya ahudhurie mahakamani kila siku shauri litakapotatwa.

Hakimu Kabate amesema, mshtakiwa ana heshima zake kwenye jamii kwa kuwa anaheshima zake, anatakiwa adhaminiwe na watu wawili wenye heshima zao na watu wawili, mmoja kati yao anatakiwa atoke sehemu moja wapo aidha Bongo movie au Tasnia ya Muziki.

“Barua zao lazima ziwe na baraka za Baraza la Sanaa Basata na kusaini bondi ya laki tano kila mdhamini,” amesema

Shauri hilo limeahirishwa hadi tarehe 12 Agosti 2020 ambapo hadi shauri hilo linaahirishwa mtuhumiwa hajatimiza masharti ya dhamana yake.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV na mitandao yetu ya kijamii kwa habari na taarifa mbalimbali

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!