Saturday , 22 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Bunge la Uturuki lapitisha sheria tata
Kimataifa

Bunge la Uturuki lapitisha sheria tata

Jengo la Bunge la Uturuki
Spread the love

BUNGE la Uturuki limepitisha sheria tata, ambayo inaipa serikali ya nchi hiyo mamlaka ya kuingilia maudhui kwenye mitandao ya kijamii na hata kulazimisha kuondolewa. Shirika la Habari la Aljazeera linaripoti…(endelea).

Kwenye sheria hiyo iliyopitishwa leo tarehe 29 Julai 2020, mitandao ya kijamii mikubwa duniani ikiwemo facebook na twitter, imelazimishwa kuwa na wawakilishi wake nchini humo.

Na kwamba, wawakilishi hao lazima wawe wenye kutii sheria za mahakama ya nchi hiyo, na pale itakapoagizwa kuondoa maudhui kwa mujibu wa sheria hiyo, itii.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, ambao watakwenda kinyume na watakumbana na hukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuondolewa maudhui yao, matangazo na kufungwa kabisa.

Sheia hiyo inatajwa kuwalenga watu zaidi ya milioni moja wanaotembelea mitandao hiyo kila siku nchini humo.

Sheria hiyo inaelekeza kuwa, wamiliki wa mitandao hiyo lazima watengeneze seva ya data ndani ya ardhi ya taifa hilo.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan

Taasisi za Haki za Binadamu na wapinzani nchini humo, wameeleza wasiwasi wao kuwa sheria hiyo ni kuminya na uhuru wa kujieleza.

Wameeleza, vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu vimekuwa vingi chini ya utawala wa Rais Recep Tayyip Erdogan.

“Kwanini sasa hivyi,” amehoji Yaman Akdeniz, professor katika Chuo Kikuu cha Istanbul’s Bilgi “mbona vyombo vyote vya utangazaji vipo chini ya serikali?”

Prof. Akdeniz amesema, mitandao ya kijamaa ni uwanja mwembamba uliobaki kwa watu kujieleza kwa uhuru nchini humo.

“Mitandao ya kijamii ni uwanda unaohifadhi maudhui kwa maisha yote, watu wengi wanatumia kupata wanachokitaka, hivyo hii sheria ni alama ya kutaka kuturudisha katika zama za giza,” amesema Tom Porteous, Naibu Mkurugenzi wa Programu Marekani nchini humo.

Hata hivyo, Ibrahim Kalin ambaye ni Msemaji wa Ikulu ya nchini humo amesema, sheria hiyo inalenga kuweka utaratibu maalumu wa kuimarisha masuala ya kibiashara kupitia kurasa hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Mwanajeshi amuua mchungaji baada ya kumfuma na mkewe kitandani kwake

Spread the loveHali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti...

Habari za SiasaKimataifa

Mmoja afariki, 30 wajeruhiwa maandamano Kenya

Spread the loveMtu mmoja ameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

error: Content is protected !!