May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwamuzi aliyekataa bao la Yanga dhidi ya Namungo afungiwa

Spread the love

Mwamuzi msaidizi namba moja Abdulaziz Ally aliyechezesha mchezo wa Namungo Fc dhidi ya Yanga ameondelewa kwenye orodha ya waamuzi kwa michezi mitatu mara baada ya kumudu mchezo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo namba 257, ulichezeshwa Jumamosi ya tarehe 13 Mei, 2021 kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa, Lindi na kumaliza kwa suluhu ya bila kufungana.

Maamuzi hayo yametolewa hii leo na kamati ya uwendeshaji na usimamizi wa Ligi (kamati ya saa 72) kwa kuzingatia kanuni ya 40:1(2.1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa waamuzi.

Mwamuzi huyo amekumbana na adhabu hiyo mara baada ya kukataa bao la Yacouba Sogne aliyeunganisha kona ya Saido Ntibanzokiza.

Katika hatua nyingine kamati hiyo imeitoza faini kya shilingi 500,000 klabu ya Yanga kwa kosa la kuingia Uwanjani kupitia mlango wa mashabiki badala ya malango maalumu kwenye mchezo dhidi ya Namungo.

Adhabu hiypo pia imetolewa kwa kuzingatia kanuni ya 45(1) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

error: Content is protected !!