April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtuhumiwa azidunda kortini kupinga masharti ya dhamana

Daniel Njonjo, Mtuhumiwa wa shtaka la kufanya vurugu Kenya

Spread the love

DANIEL Njonjo, anayetuhumiwa kwa shtaka la kufanya vurugu, amepigana na polisi katika korti ya Mahakama ya Milimani jijini Nairobi, Kenya, akipinga sharti la dhamana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kisa hicho kimetokea jana tarehe 8 Januari 2020, baada ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Muthoni Nzibe, kumuamuru mtuhumiwa huyo kutoa Shilingi ya Kenya 30,000, kama sharti la dhamana.

Baada ya mahakama kutoa sharti hilo, Njonjo alianza vurugu na kupelekea kupigana na maafisa polisi wa mahakama hiyo, waliojaribu kumkamata kwa ajili ya kumpeleka rumande.

Katika utetezi wake, Njonjo alisema ni bora afe kuliko kutekeleza sharti hilo, kwa kuwa hana uwezo wa kutoa kiasi hicho cha fedha.

Na kuiomba mahakama hiyo kumuacha kwa dhamana, kwa kuwa hakumuuwa mtu.

Njonjo anatuhumiwa kukutwa na kisu katika Mtaa wa Kimathi jijini Nairobi, Kenya. Na anatarajiwa kurudi tena mahakamani hapo tarehe 22 Januari mwaka huu, siku ambayo kesi yake itakwenda kutajwa.

error: Content is protected !!