April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kocha wa Hazard atua Yanga, kuanza na Kombe la Mapinduzi

Luc Eymael, Kocha Mpya wa Yanga

Spread the love

UONGOZI wa Yanga leo umemtangaza, Luc Eymael, Raia wa Ubelgiji kuwa kocha mkuu wa timu hiyo na moja kwa moja atajiunga na kambi ya timu hiyo iliyoko Zanzibar kwenye michauno ya Kombe la Mapinduzi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kocha huyo ambaye amewafundisha Eden Hazard nchini Ubelgiji, ametua nchini na mchana anatarajia kwenda Unguja kushuhudia mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 2:15 usiku kwenye uwanja wa Amani.

Luc ambaye amefundisha klabu mbalimbali barani Afrika kama, AS Vital (Congo), Missile (Gabon), MC Oran (Algeria), AFC Leopards (Kenya), Rayon Sport (Rwanda), Orlando Pirates (Afrika Kusini), JS Kairouan (Tunisia), Al Merrikh ya kutoka Sudan, Free States na Black Leopards zote za Afrika Kusini .

Kocha huyo amekuja kuchukua mikoba ya Mwinyi Zahera aliyetupiwa vilago mwishoni mwa mwaka jana, huku timu hiyo ilikuwa chini ya kocha wa muda Boniface Mkwasa.

error: Content is protected !!